Gloria Muliro aonesha picha akifurahia mandhari ya Marekani

Muhtasari

• Msanii wa injili Gloria Muliro ameweka picha za kupendeza akijivinjari kwenye majira ya baridi huko Marekani.

• Muliro, ambaye alifanya harusi yake na mhandisi na mhubiri Evans Sabwami mwisho mwa mwezi Oktoba waka 2021 anaonekana akifurahia mandhari hayo ya theluji

Gloria Muliro
Image: Facebook

Msanii wa injili Gloria Muliro ameweka picha akijivinjari kwenye majira ya baridi huko Marekani.

Muliro, ambaye alifanya harusi yake na mhandisi na mhubiri Evans Sabwami mwisho mwa mwezi Oktoba waka 2021 anaonekana akifurahia mandhari hayo ya theluji huku akifuatisha mrundiko wa picha hizo na maandishi mafundi,

“Msimu wa baridi upo huku kwa ujasiri

Theluji ilianguka

Ina uzuri wake!”

Aliandika Muliro kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwenye mrundiko wa picha akiwa kwenye theluji, Gloria ameonekana akifanya shughuli mbali mbali kama kupangusa theluji kutoka kwa gari, kuokota theluji, kukimbia kwenye theluji miongoni mwa mambo mengine huku akiwa na kufurahia mno.

Mwezi Oktoba mwaka 2021, msanii huyo alifunga ndoa na mpenzi wake mhubiri na mhandisi Evans Sabwami.

 Harusi hiyo ya kifahari iliyodhuriwa na familia pamoja na marafiki wa karibu jijini New York, siku chache baada ya kufanya tamasha lingine Eldoret nchini Kenya.

Mashabiki wa msanii Gloria Muliro walimpongeza kwa hatua hiyo kubwa ya kufunga harusi na mchungaji Sabwami, haswa baada ya ndoa yake ya awali na mhubiri Eric Omba kuvunjika miaka sita iliyopita.