Khadija Kopa amshauri bintiye Zuchu anapokaribia kuasi ukapera

Muhtasari

Khadija Kopa amempa ushauri mwanawe Zuchu ambaye anakaribia kuasi ukapera mwezi huu

•Khadija Kopa ameeleza kuwa mwanawe  amemlea kwa madili mema hivyo hana shaka naye kuwa atakuwa mke mwema kwa bwanake na kamwe anamini hatamwaibisha kwa hatua ambayo ameamua kuichukua. 

Khadija Kopa na mwanawe Zuchu
Khadija Kopa na mwanawe Zuchu
Image: Hisani

Staa wa taarabu nchini Tanzania Khadija Kopa amempa ushauri mwanawe Zuchu ambaye anakaribia kuasi ukapera mwezi huu.

Ni habari ambazo zimekuwa zikitikisa vichwa, mitandaoni, wanablogi wakipata kazi huku vyombo vya habari vikidakia udaku pia.

Kupitia ukurusa wa instagram, Khadija Kopa ameeleza kuwa mwanawe  amemlea kwa madili mema hivyo hana shaka naye kwamba atakuwa mke mwema kwa bwanake na kamwe anaamini hatamwaibisha kwa hatua ambayo ameamua kuichukua. 

"Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti Mungu akakusimamie najua hutoniangusha," alisema Khadija Kopa kwa bintiye Zuchu.

Inatarajiwa tarehe 14 Februari itakuwa siku ya ndovu kumla mwanawe ambapo Zuchu na Diamond watakuwa wanafunga ndoa  rasmi na kufikisha kikomo  tetesi ambazo zimekuwa zikienezwa kwenye mitandao  ya kijamii.

Ikumbukwe Mama Dangote alipakia video iliyokuwa ikionyesha Diamond na Zuchu wakiwa kwenye harusi ambapo aliambatinisha na ujumbe kwamba amethibitisha ndoa ya wawili hao.