Mwanasosholaiti Vera Sidika afunguka kuhusu uhusiano wake na mama mkwe wake

Muhtasari

•Vera alisema kuwa mama ya mumewe Brown Mauzo anapendelea sana kumjulia hali na huwa wanawasiliana mara kwa mara.

•Mwanasholaiti huyo pia alifichua anapanga kupata mtoto mwingine mwaka ujao.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri Vera Sidika amedhihirisha kuwa kuna uhusiano mzuri kabisa katika familia yake.

Alipokuwa anashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu, Vera aliweka wazi kwamba kuna maelewano mazuri kati yake na mama mkwewe.

Mwanasoshalaiti huyo alisema kuwa mama ya mumewe Brown Mauzo anapendelea sana kumjulia hali na huwa wanawasiliana mara kwa mara.

"Uhusiano ni mzuri. Huwa tunaelewana na wakati niko na shughuli nyingi huwa nasahau kumpigia simu. Kila siku huwa anapiga simu kunijulia hali" Vera alijibu shabiki aliyetaka kufahamu kuhusu uhusiano kati yake na mama mkwe.

Mama huyo wa mtoto mmoja pia alifichua kuna upendo mkubwa kati yake, mumewe na binti yao Asia Brown.

Vera alisema kuwa kila siku yeye na mumewe wamekuwa wakionyeshana upendo mkubwa kama wanandoa na kwa pamoja wanampenda sana binti yao.

"Kitu cha kwanza yeye (Brown Mauzo) huwa ananibusu kwenye paja la uso na kwenye midomo 'asubuhi njema mpenzi wangu' kisha anambusu Asia kwenye mashavu. Siwezi kuhesabu mara ambazo huwa anatasema 'nawapenda'. Huwa anasema mara kwa mara siku nzima.. Nadhani anampenda binti yetu sana kuniliko. Hawawezi kutenganishwa. Na jinsi ninavyompenda (Asia) kishenzi" Alisema.

Mwanasholaiti huyo pia alifichua anapanga kupata mtoto mwingine mwaka ujao. Alisema anakusudia kupata jumla ya watoto wanne, wasichana wawili na wavulana wawili.