Sina mtoto mwingine ni Asia tu,'Vera Sidika azungumzia madai ya kumficha kifungua mimba wake

Muhtasari
  • Hisia za Vera zinakuja baada ya shabiki mmoja kuhoji iwapo ana mtoto mwingine kando na Asia Mauzo
  • Sidika alikuwa wa kwanza kutupilia mbali madai yaliyotolewa dhidi yake hadharani kwenye mitandao ya kijamii
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mfanyibiashara na mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika amekanusha madai kwamba anamficha mtoto wake wa kwanza kutoka kwa umma.

Hisia za Vera zinakuja baada ya shabiki mmoja kuhoji iwapo ana mtoto mwingine kando na Asia Mauzo.

Sidika alikuwa wa kwanza kutupilia mbali madai yaliyotolewa dhidi yake hadharani kwenye mitandao ya kijamii.

Vera alisisitiza kuwa ana Asia tu na kwamba angekuwa na mtoto mwingine angekuwa anampakia mitandaoni kama mwanawe Asia kwani ana upend mwingi kwa watoto.

Alijibu hayo kwenye sekta ya insta stories ambapo shabiki wake alimuuliza kama anamtoto mwingine kama invyodaiwa, ambapo alikana madai hayo na kusema kuwa;

"Ningeweza aje kuwa na mtoto mwingine na nyinyi nyote mkose kujua,napenda watoto sana angekuwa kwenye mitandao ya kijamii kama Asia, pia natamani kumpata mtoto kijana," Vera Alijibu.

Pia aisema kuwa atampata mtoto mwingine mwaka ujao, na anatazamia kuzaa watoto wanne.