Zuchu amuomba Diamond kuzungumzia uhusiano wao

Muhtasari
  • Zuchu alijipata kwenye mahojiano moto  aliyotakiwa kueleza mashabiki wake kama ni kweli anachumbiana na bosi wake Diamond Platnumz
  •  Zuchu aliagizwa kuelezea ukaribu wake  na bosi wake, Diamond. Maneno ambayo yalimfanya aonekane kama kashikwa na kigugumizi ila mwishowe akajibu kwa kusema anayepaswa kulizwa swali hilo ni bosi wake
Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: hisani

Msanii  kutoka Tanzania Zuchu alijipata kwenye mahojiano moto  aliyotakiwa kueleza mashabiki wake kama ni kweli anachumbiana na bosi wake Diamond Platnumz.

Akiwa katika kituo kimoja cha  habari, Zuchu alitakiwa kuelezea ukaribu wake  na bosi wake, Diamond. Maneno ambayo yalimfanya aonekane kama kashikwa na kigugumizi ila mwishowe akajibu kwa kusema anayepaswa kuulizwa swali hilo ni bosi wake.

Aliongeza kwa kuimba wimbo uliokuwa ukiomba mpenzi wake huyo aweke mambo wazi ili mahasidi wakose la kuongea.

"Ukitaka uniweze fanya wazi wakuone, mahasidi wanyamaze wasiseme wala wanong'one, hunny wangu jamani fanya hima wakuone,"aliimba Zuchu.

Zuchu alijiunga na Wasafi mwaka 2020 ambapo amekuwa akitoa nyimbo sifika, baadhi  ya nyimbo zake zinazopendwa sana na mashabiki wake ni; Sukari, nyumba ndogo, cheche  na  ya hivi karibuni mwambieni.

Ilikuwa imesubiriwa kwa hamu na ghamu kuwa mwanamuziki huyo angeweka mambo wazi kuhusu mahusiano baina yake na Diamond ila alikwepa kulizungumzia swala hilo.

Kinachobuliwa  sasa ni tarehe 14 ambapo ametaja kuwa  siku muhimu kwake ambapo atakuwa anatambulisha mpenzi hadharani.