Nakuwaza, nimekukosa,'Mwanasosolaiti Manzi wa Kibera amwambia meneja wake

Muhtasari
  • Manzi wa Kibera amekuwa akivuma mitandaoni kwa ajili ya mambo tofauti, huku akivuma mara ya kwanza baada ya kuzua vita kati yake na mwanasosholaiti Shakilla
Manzi wa Kibera
Image: Hisani

Kama umekuwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii, mwanasosholaiti chipukizi Mani wa KIbera sio mgeni kwa wengi.

Manzi wa Kibera amekuwa akivuma mitandaoni kwa ajili ya mambo tofauti, huku akivuma mara ya kwanza baada ya kuzua vita kati yake na mwanasosholaiti Shakilla.

Muda usiokuwa mrefu Manzi wa kibera alifunga pingu za maisha na Chali wa KIera ambapo walitengana baada ya muda mfupi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, mwanasosholaiti huyo ameibua hisia tofauti baada yakupakia video akiwa anambusu mwanamume huyo na  kusema jinsi anavyompeza, na kujihisi akiwa karibu naye.

"Jinsi ninavyojihisi nikiwa na wewe❤️💕😭 @chali_wa_kiberanajua umekuwa meneja wangu lakini baada ya kila kitu Siwezi Kuacha Kuwaza Juu Yako," Aliandika Manzi wa KIbera.

Hivi majuzi akiwa kwenye mahjiano alisema kwamba amekuwa akitumia dawa za kuongeza makalio yake.