Nilizimia! Baada ya kuniambia ana virusi vya ukwimi-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Kuwa na virusi vya ukwimwi sio mwisho wa dunia katika maisha yako au mwisho wa kutabasamu na kuwa na furaha kwani kuna wengi ambao wanapata matibabu

Ni jambo lipi abalo umewahi sikia au kupitia mpaka ukajihisi kwamba uanataka wakati wako hurudi na nyuma ili kufanya maamuzi yako upya?

Kuwa na virusi vya ukwimwi sio mwisho wa dunia katika maisha yako au mwisho wa kutabasamu na kuwa na furaha kwani kuna wengi ambao wanapata matibabu.

Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na mwwanamume mmoja ambaye alinisimulia masaibu ambayo amepotia kwenye maisha yake baada ya kukutana na aliyekuwa mpenzi wakee.

Huu hapa usimulizi;

"Miaka 15 iliyopita nilipatana na msichana mrembo kweli, unajua vile mambo ya wanaume hukua akipendezwa na mwanamke alinipenda na mimi nikampenda

Tulichumbiana kwa muda wa wa miaka 3, siku ambayo niliamua kuenda kumtambulisha kwetu ili tuanze au tuvuke kwenye maandalizi ya ndoa

Siku moja aliamka na kuniambia kwamba ana virusi vya ukimwi, nilizimia kwani nimekuwa nimelala naye kwa miaka 3 ilhali hajawahi niambia chochote

Ushauri wangu kwa wanandoa wachanga ni kuwa kabla ya kuanza uhusiano wenu mnapaswa kuenda kupimwa ili kuhakikisha kila mmoja yuko salama

Pia kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa dunia, wala maisha kwani ninaishi na furaha hata baada ya kuwa na virusi hivi."