Karen Nyamu aibua mdahalo kuhusu ujauzito wake

Muhtasari

• Karen alikuwa akijibu shabiki mmoja aliyezua madai kwamba Samidoh alikana ujauzito wa mwanasiasa huyo.

 

Mwanasiasa Karen Nyamu Picha: RADIO JAMBO
Mwanasiasa Karen Nyamu Picha: RADIO JAMBO

Mwanasiasa na Baby mama wa Samidoh, Karen Nyamu siku ya Jumatatu aliibua mdahalo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoa kauli iliyotafsiriwa na wanamitandao  kuwa alikana madai kuwa Samidoh ndiye baba wa mtoto anayetarajia siku za  hivi karibuni.

Karen alikuwa akijibu shabiki mmoja aliyezua madai kwamba Samidoh alikana ujauzito wa mwanasiasa huyo.

Wawili hao wiki jana walirushiana cheche za maneno kila mmoja akionekana kutumia misemo kumkabili mwenzake.

Karen Nyamu kupitia ukurusa wake wa Instagram alikana madai hayo na kuongeza kuwa ujauzito alionao si wa mwanamuziki huyo nguli wa Benga.

“Acheni kujishuku, hajaambiwa mimba ni yake”alisema Karen Nyamu.

Kwa mashabiki ambao wamekuwa wakifuatilia mwanasiasa huyo kwa karibu wameshangazwa na kauli yake kwani yeye ndiye alitangaza kuwa Samidoh alimpa ujauzito Agosti mwaka jana baada ya wawili hao kuzozana.