Maina Kamanda pichani na Millicent Omanga baada ya video ya kumbato na Elachi

Seneta mteule Millicent Omanga na Mbunge wa zamani wa Starehe, Maina Kamanda
Seneta mteule Millicent Omanga na Mbunge wa zamani wa Starehe, Maina Kamanda
Image: Facebook

Seneta mteule Millicent Omanga amepiga jeki mjadala unaoenezwa mitandaoni kutokana na picha iliyovujishwa ikimuonesha aliyekuwa spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi, akiwa anamshikilia aliyekuwa mbunge wa Starehe Maina Kamanda kwa njia ya kumhendo kimahaba.

Picha hiyo inayomuonesha Elachi akiwa amemzunguka kiunoni Kamanda kwa mikono yake yote katika njia inayoakisi huba zito.

Video hiyo iliyosambazwa sana inaarifiwa kutoka kwa wanachama wa muungano wa Azimio la Umoja wakati walikuwa na mkutano na wanahabari katika uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi.

Kamanda na Elachi walionekana kujisahau kabisa mpaka ikambidi mbunge wa Kibera Imran Okoth kuwadokezea kwamba walikuwa wanarekodiwa video wakiwa wameshikana.

Jumanne asubuhi pia Omanga alipakia picha akiwa amewekelea mkono wake kwenye bega la Kamanda, huku mbunge huyo wa zamani akionekana kufurahia mpaka kuyatoa meno yote nje kwa tabasamu.

Ukiitazame video hiyo na kulinganisha matukio hayo na picha aliyoipakia Omanga, bila shaka utapata kujijibu maswali mengi mwenyewe.