Stephen Letoo amfokea shabiki, "Mimi si shoga!"

Muhtasari

• "Mimi so long as madem wananipenda. Wababa kama wewe mnaweza kwenda huko mimi si shoga" - Stephen Letoo amjibu shabiki anayetaka asiwe na upendeleo katika kuripoti ili apendwe na wote.

Mwandishi wa habari Stephen Letoo
Mwandishi wa habari Stephen Letoo
Image: Facebook

Mwandishi wa habari Stephen Letoo wikendi iliyopita aliwaacha mashabiki wengi katika kicheko kikubwa baada ya kuchukua ujasiri uliopitiliza na kumjibu shabiki wake mmoja aliyemtaka kutoegemea pande yoyote wakati anaripoti habari.

Letoo ambaye ni mwandishi wa habari katika kituo kimoja cha runinga nchini alipashwa na shabiki huyo ambaye alidai kwamba Letoo anaegemea baadhi ya marengo ya kisiasa anaporipoti matuio ya kisiasa nchini.

Shabiki huyo aidha alitoa wosia kwa Letoo kwamba akitaka apendwe zaidi basi ni sharti aache kuegemea pande fulani za kisiasa, haswa mwaka huu ambapo matukio ya kisiasa ni mengi na Letoo ndiye anaaminiwa kuripoti matukio hayo

Kilichoshangaza wengi ni kwa jinsi Letoo alimjibu shabiki huyo huku akimwambia kwamba hana haja ya kupendwa na wanaume kama yeye kwani yeye si shoga. Vile vile Letoo alimjibu akasema kwamba bora anapendwa na wanawake, ni sawa kwake.

Letoo alikuwa amepakia picha akiwa na wenzake kando ya barabara ambapo alieleza kuwa ni Busia walipoenda kufuatilia matukio ya mkutano wa kisiasa, na akaelezea jinsi walikuwa wanakimbizana na muda kurekodi taarifa ili kusomwa katika habari za saa moja jioni.

Katika post hiyo ambapo alionekana kuelezea masaibu waandishi wa habari hupitia nyanjani wanapotafuta habari huku wakikimbizana na muda, ndipo shabiki huyo alijitoma na kuachia maoni yake.

“Stephen Letoo, natamani ungekuwa mtaalamu tu na usiwe na upendeleo. Unaweza kupendwa na kila mtu. Jaribu na usiwe upande wowote,” aliandika shabiki huyo.

“Mimi so long as madem wananipenda. Wababa kama wewe mnaweza kwenda huko mimi si shoga,” alijibu kwa ukali Letoo.

Hapa wapenzi wa ubashiri walisema pande zote mbili zilifungana mabao!