'Udhaniye Siye Ndiye,'Bahati amlimbikizia sifa Ringtone

Muhtasari
  • Hii ni baada ya Ringtone kujitokeza kwa manifesto yake na pia hafla ya kuchangisha pesa ambayo ilikuwa hafla ya kibinafsi na ilitokea katika hoteli moja ya bei ghali jijini Nairobi
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Bahati

Msanii Kevin Bahati, mbunge anayetarajiwa kuwa mbunge wa Mathare amejitokeza wazi kumsifu msanii wa injili mwenye utata zaidi nchini Kenya Ringtone Apoko.

Bahati amemtaja Ringtone kama Mwenyekiti asiyeshindwa wa Muziki wa Injili nchini Kenya.

Hii ni baada ya Ringtone kujitokeza kwa manifesto yake na pia hafla ya kuchangisha pesa ambayo ilikuwa hafla ya kibinafsi na ilitokea katika hoteli moja ya bei ghali jijini Nairobi.

Ada ya kiingilio ilikuwa ksh. 100,000 kwa kila meza, ndiyo maana lilikuwa tukio la faragha, kwa watu wenye pesa tu.

"Udhaniye Siye Ndiye!!! Asante sana Mwenyekiti @RingtoneApoko kwa kuhudhuria na Kuunga mkono Uzinduzi Wa Ilani Yangu Jana. Mathare Haitafanana Tena!

Sitasema Mengi Ila Nakuidhinisha Rasmi Uwe Mwenyekiti Wa Injili Bila Kushindwa ," Aliandika Ringtone.