"Huyu sasa ndiye wa maisha!" Babake Diamond amkubali mpenzi wake mpya

Muhtasari

•Amemtakia mwanawe mema katika ndoa yake na kutangaza wazi kuwa angependa mpenzi huyo mpya wa Diamond  awe mkewe wa maisha.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Baba wa kambo wa Diamond Platnumz, Uncle Shamte ameeleza kuridhishwa kwake na mpenzi mpya wa staa huyo wa Bongo.

Uncle Shamte ambaye ni mume wa sasa wa Mama Dangote ameweka wazi kwamba amempokea malkia huyo ambaye hajatambulishwa kwa mikono miwili.

Amemtakia mwanawe mema katika ndoa yake na kutangaza wazi kuwa angependa mpenzi huyo mpya wa Diamond  awe mkewe wa maisha.

"Siwezi kusema atakuwa Mke wa Uji ila Leo umenidhihirishia ukubwa wako Simba, akawe wa milele🙌 huyu sasa ndio wa Maisha nimempokea kwa mikono miwili🤲 Kwa alivyonyooka hivi atakuwa wa wapi huyu?" Shamte alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Shamte anaunga mkono kauli ya mkewe, Mama Dangote ambaye alimshauri Diamond afunge pingu za maisha na kipenzi hicho chake kipya.

Mama Dangote alieleza kuridhishwa kwake na mwanadada huyo asiyetambulishwa na kumpokea katika familia yake kwa mikono miwili.

"Nashindwa kuelezea furaha yangu mwanangu, Naseeb Diamond Platnumz🦁, hapa sasa umepata mwenza. Utulie babangu uoe," Mama Dangote alisema.

Jumbe za wanandoa hao wawili zimeibua tetesi kwamba huenda Diamond alifunga ndoa kisiri. Wengi wanasubiri kwa hamu kumtambua malkia mpya kwenye ufalme wa Simba.