PICHA YA SIKU:Kutana na mwanawe Diamond anayefanana naye kama shilingi kwa ya pili

Muhtasari
  • Kutana na mwanawe Diamond anayefanana naye kama shilingi kwa ya pili
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM

Wanamitandao walimbandika staa wa bongo Diamond Platnumz jana la 'Father Abraham' kutokana na kuwa na baby mama wengi.

Safari ya muziki ya msanii huyo inafahamika vyema na wanamitandao, kwani alianza usanii wake akiwa kijana mdogo.

Mwezi jana msanii huyo alifihua kwamba anaweza kuwa na watoto 5 au 6, huku akidai kwamba ana mtoto na mwanamke ambaye yuko kwenye ndoa.

Uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na msanii Tanasha Donna haukudumu sana kwani  wawili hao waliachana miezi chache baada ya kubarikiwa na kifungua mimba wao Naseeb Junior.

Unapotazama picha ya mwanawe Diamond Naseeb kwa hakika utasema kuwa ni pacha wake Diamond.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Tanasha alipakia picha yake na mwanawe, ambapo mashabiki hawakuweza kulaza damu bali alimsifia mwanawe Tansha huku wakisema kwamba anafanana na baba yake kamili na kuwa ni picha wake.

Hizi apa baadhi ya picha zinazoonyesha kuwa Naseeb ni pacha wa baba yake kamili.

Image: Tanasha Donna/INSTAGRAM