Haikuwa kiki-Mpenzi wake Nicah The Queen aweka mambo wazi baada yao kurudiana

Muhtasari
  • Mpenzi wake Nicah The Queen aweka mambo wazi baada yao kurudiana
Nicah the Queen na mchumba wake
Nicah the Queen na mchumba wake
Image: Instagram, KWA HISANI

Mwinjilisti Nicah the Queen kwa mara nyingine tena amerudiana na mpenzi wake mzalishaji wa muziki na mcheza santuri Slahver, siku chache tu baada ya kutangaza kwamba wamefikia maamuzi ya kuachana.

Baadhi ya wanamitandao walisema na kudai kamba wawili hao wanatafuta kiki, na kwamba walikuwa wanatafuta kiki kwani waliachana kwa siku chache na kurudiana huku mapenzi yao yakionekana kunoga kila siku.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram wa Slahver alikanusha madai ya kutafuta kiki, na kuweka wazi kwamba walikuwa wameahana na mpenzi wake kwa siku 9.

"Mapenzi ni jambo nuri na linakuja na nyakati tofauti,kama wapenzi wachanga huwa tunakubaliana na kutokubaliana kwa mambo kadhaa kwani tuko katika msafara wa kujuana na kusoma kila mmoja wetu

Kwa hivyo hatukuwa tunatafuta kiki au kutafuta umakini kwani tulikuwa tumeachana kwa siku 9,Asanteni kwa wale ambao walituombea wakati wa kutengana kwetu, kile mtu ameleta pamoja." Aliandika Slahver.