Umezidi sasa-Wanamitandao wamwambia Harmonize baada ya kununulia Kajala Range Rover mbili

Muhtasari
  •  Mwimbaji huyo amejipatia jina la 'mfalme wa simps' kutokana na kuendelea kumtaka mpenzi wake wa zamani
Harmonize na mwigizaji Fridah Kajala Masanja
Harmonize na mwigizaji Fridah Kajala Masanja
Image: HISANI

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Harmonize amekuwa akijaribu kila juhudi ili Kajalaaweze kumrudia  kwa muda mrefu sasa.

Harmonize ametoa pole nyingi hadharani kwa Kajala lakini bado hajafanikiwa kurejesha mwigizaji huyo kwenye maisha yake.

 Mwimbaji huyo amejipatia jina la 'mfalme wa simps' kutokana na kuendelea kumtaka mpenzi wake wa zamani.

Hatua ya hivi punde zaidi ya Harmonize imekuwa ya kupata magari mawili ya hali ya juu katika jaribio la kumrejesha Kajala.

Katika video aliyoiweka, Harmonize alifichua Range Rover mbili ambazo inadaiwa alimnunulia Kajala.

Range Rover nyeusi na nyeupe yenye jina laKajala.

Watu wameguswa na hatua ya hivi punde ya Harmonize na wengine wanamtaka Kajala kuwa binadamu na akubali msamaha wa aliyekuwa mpenzi wake.

Wengine wanamshauri Harmonize aendelee na kuzingatia brand yake badala ya kupoteza muda kujaribu kumrudisha Kajala.

Wanamitandao hawajasalia nyumba bali wameweza kumshambulia mwanamuziki huyo na kusema kuwa amezidi  sasa.