Binti ya Elon Musk ataka kubadili jina kuepuka uhusiano na baba yake

Muhtasari

•Bintiye Musk ameiomba mahakama ibadili utambulisho wa jinsia yake kutoka ya kiume na kuwa ya kike na kumsajiri kwa jina jipya, 

•Jina lake jipya liliondolewa katika waraka wa mtandao

Image: ELON MUSK

Binti wa tajiri Elon Musk aliyebadili jinsia yake amewasilisha ombi la kubadilisha jina lake kulingana na utambulisho wa jinsia yake mpya na kwasababu anasema "Siishi au nisingependa kuwa na uhusiano na baba yangu mzazi kwa njia yoyote ile, kwa umbo au muundo ."

Ombi la kubadilisha majina yake yote mawili na kupata cheti kipya cha kuzaliwa kinachoonyesha utambulisho wa jinsia yake mpya liliwasilishwa kwa Mahakama ya juu zaidi ya Kaunti ya Santa Monica mwezi Aprili. Taarifa hii ilijulikana hivi karibuni kupitia baadhi ya mitandao ya habari ya kijami.

Mtoto huyo Bw Elon Must ambaye awali alijulikana kama Xavier Alexander Musk, ambaye hivi karibuni alitimiza umri wa miaka 18, umri ambao ni umri wa utu uzima katika California, ameiomba mahakama ibadili utambulisho wa jinsia yake kutoka ya kiume na kuwa ya kike na kumsajiri kwa jina jipya, kulingana na nyaraka za mahakama zinazopatikana kupitia mtandao wa PlainSite.org.

Jina lake jipya liliondolewa katika waraka wa mtandao. Mama yake ni Justine Wilson, ambaye alitaliakiana na Musk mwaka 2008.

Hakuna maelezo kuhusu nini kilichosababisha kutoelewana baina ya Bw Musk na binti yake.