“Kuondoa Mabango Haswa Kama Umepoteza ni Uchungu akini ni Jambo sahihi kufanya,” Boniface Mwangi

Mwangi aligombea ubunge Starehe 2017 lakini akashindwa na mbunge anayeondoka Charles Njagua.

Muhtasari

• Mwangi alisema kwamba anajua kwa sababu alikuwa katika hali kama hiyo mwaka 2017 alipowania ubunge ila akashindwa.

Boniface Mwangi, Bango la matangazo
Boniface Mwangi, Bango la matangazo
Image: Facebook

Mwanaharakati Boniface Mwangi ambaye amekuwa akiupigia upato muugano wa Azimio la Umoja One Kenya kushinda haswa katika wadhfa wa urais amewataka wanasiasa ambao walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliokamilika mapema wiki hii kwenye sehemu nyingi nchini kuanza mchakato wa kutoa mabango yao yote ili kutoa nafasi kwa biashara zingine kujitangaza kweney nafasi hizo za mabango ya umma.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mwangi amewarai wanasiasa hao kukubali na kusonga mbele kwani kuna maisha baada ya uchaguzi na nafasi hizo ambazo wametundika mabango yao zinahitajika kutumika kutangaza biashara zingine.

Mwangi aliyaandika haya kufuatisha Tweet yake ya mwaka 2017 ambapo alisema alichukua picha hiyo pamoja na wafuasi wake baada ya kuyaondoa mabango ya kampeni zake eneo bunge la Starehe jijini Nairobi alikokuwa akiwania katika uchaguzi huo ila akashindwa na Charles Njagua.

“Likizo fupi ya selfie na watu waliojiunga nami kuondoa mabango yangu ya kampeni. Kuna timu zingine kwenye mitaa zinafanya kazi sawa. Ewe mwaniaji, iwe ulishinda au ulishindwa, tafadhali panga ili mabango yako ya kampeni yaondolewe. Acha kuta na miti jinsi ulivyoipata,” Mwangi aliwarai wanasiasa wote ambao wametundika mabango yao ya kampeni katika sehemu mbali mbali nchini.

Vile vile, Mwangi alidokeza kwamba anajua ni uchungu na aibu kutoa mabango hayo, haswa kwa mwaansiasa aliyepoteza, kwa sababu alijikuta katika hali kama hiyo mwaka 2017 baada ya kupoteza uchaguzi ila akasema ndicho kitu kizuri sana utafanya kama ulipoteza.

“Kuondoa mabango yako haswa ikiwa umepoteza ni mchakato chungu lakini ni jambo sahihi kufanya,” Mwangi alishauri.

Mwanaharakati huyo mwenye misimamo mikali aliposhindwa katika uchaguzi wa 2017, baadae alishiriki katika filamu yake ya Softie ambapo katika kipengee kimoja kweney filamu hiyo alisikika na kuonekana akidokeza kwamba hana mpango wala hawezi tena kujihusisha kwenye siasa kama mgombeaji.