(+video) Mwalimu Anayepiga Mbizi Kuvuka Mto ili Kuwahi Shuleni Kila Siku

Mwalimu Mensah anapiga mbizi mtoni kuvuka kila siku ili kuwahi shuleni kuwafunza watoto.

Muhtasari

• Alisema hata familia yake inabaki na wasiwasi iwapo atarudi jioni kwa sababu wanajua ni lazima avuke mtoni kwa kupiga mbizi ili kufika upande wa pili na kurudi.

Mwalimu Mensah Kwame akivuka mto kwa kupiga mbizi
Mwalimu Mensah Kwame akivuka mto kwa kupiga mbizi
Image: Screengrab//Youtube//TV3

Hadithi ya mwalimu mkuu mmoja katika shule ya msingi nchini Ghana ni moja ya kutia matumaini sana baada ya kugundulika kwamba mwalimu huyo mkuu anapiga mbizi katika mto ili kuvuka na kuwahi shuleni kutoa huduma ya elimu kwa watoto.

Katika hadithi hiyo iliyoangaziwa na runinga moja ya nchini humo, mwalimu huyo kwa jina Mensah Kwame katika shule moja ya msingi ambayo mandhari yake si ya kuvutia kabisa analazimika kusafiri iumbali wa zaidi ya kilomita kadhaa kutumia kipikipiki chake kikuukuu na wakati kimeharibika hulazimika kuvua nguo kando ya mto na kupiga mbizi kuvuka ili kuwahi shuleni.

Msimulizi katika hadithi hiyo anaeleza kwamba baada ya kusafiri kwa kilomita tisa, analazimika kujitoma mtoni kama Samaki ili kuvuka na kisha kuendelea na safari iliyosalia ya kilomita tatu zaidi kufika shuleni, eneo ambalo linaonesha mazingira ya shule ya kutia huruma vibaya mno.

“Kama mwalimu katika eneo hili la mashambani, ninalazimika kuamka asubuhi sana. Hata ninapoondoka, familia yangu inabaki na wasiwasi kidogo kwa sababu njiani kuna mto. Hata hawana uhakika iwapo ninavyoweza kurudi nyumbani baada ya shule," Mwalimu Mensah Kwame alielezea.

Mwalimu huyo alielezea kwamba mara nyingi anapofika katika mto huwa hakuna mtu mwenye jahazi la kuwavusha upande wa pindi na hivyo huwa analazimika kuvua nguo na kipiga mbizi mpaka upande wa pili, kuchukua jahazi na kurudi nalo upande wa kwanza kuchukua nguo zake na baadhi ya vitu vingine na kisha kuvuka tena kuendelea na safari kuelekea shuleni.

“Mara nyingi wakati tumefika kando ya mto, hakauna mashua ya kutuvusha upande wa pili, na kwa hiyo kama mwalimu inanibidi nivue nguo na kupiga mbizi upande wa pili kuleta mashua ili kuchukua vitu vyangu na kuvuka navyo tena,” Mwalimu huyo alisema.

Aidha, alisema kwamab walijaribu kuomba hifadhi karibu na eneo la shule ili kurahisisha usafirishaji wao ila ikashindikana kabisa na kwa hiyo inawabidi kusafiri kilomita kadhaa kila siku ili tu kuwafundisha wanafunzi.