(+video) Mchungaji aliyetukana waumini kwa kutomnunulia saa aomba radhi

Carlton Funderburke aligonga vichwa vya habari baada ya video kuvujishwa akiwaapiza waumini kwa maneno ya kashfa.

Muhtasari

• “Acha nishushe mlango niongee na wanangu wa kiume na wa kike wa bei nafuu." mchungaji huyo aliwakashfu waumini kwa kukosa kumnunulia saa ya mkononi.

Baada ya video ya mchungaji Carlton Funderburke, mchungaji sasa wa Kansas City ambaye aliita kutaniko lake "maskini, wavunjaji, waliovunjika na waliochukizwa" kusambaa kweney mitandao ya kijamii na kuzua ghadhabu miongoni mwa waumini kote ulimwenguni, mchungaji huyo sasa amenyenyekea na kuomba msamaha kwa kitendo hicho cha kuchukiza.

“Nataka kuchukua fursa hii ili kuzungumzia video amabyo imesambaa yangu nikifanya mahubiri wiki jana, ingawa kuna maana katika mahubiri yale, ila ningependa kuomba radhi kwa hasira na uchungu ulioletwa na maneno yangu. Nimezungumza na wale ambao ninawajibishwa nao na nimepokea marekebisho na maagizo” Mchungaji huyo alisema.

Pia alizidi kunyenyekea kwa kusema kwamab klipu ile kwa njia moja au nyingine haifai kabisa kuchukuliwa kama ndivyo anavyowatafsiri watu wa Mungu au hata kuonesha jinsi Moyo wake unavyotoa hisia dhidi ya waumini.

 “Pia nimeomba radhi kwa kanisa ambalo limesimama nami na kunionesha upendo. Klipu ile haioneshi kwa njia yoyote kuwakilisha moyo wangu au jinsi ninavyowaona watu wa Mungu,” Carlton Funderburke alisema kweney klipu nyingine iliyopakiwa pia kwenye TikTok.

Wiki jana, video ya mchungaji Funderburke akiwafokea waumini kwa kushindwa kumnunulia saa ya mkononi kupokelewa kwa njia hasi na wanamitandao, aliwaita watu wa mitumba waliokata tamaa na maskini na kujipata katika hali ya songombingo na watu ambao walimjia juu kwa maneno ya kashfa vile vile, katika kile kilichoonekana ni kukabiliana jino kwa jino.

“Acha nishushe mlango niongee na wanangu wa kiume na wa kike wa bei nafuu. Tazama ndivyo ninavyojua wewe bado ni maskini, umevunjika, umechanganyikiwa, na umechukizwa kwa sababu ya jinsi umekuwa ukiniheshimu,” mchungaji alipandwa na mori.