(+video) Mwanadada atupa paka chini na kukimbia alipogundua ana panya mdomoni

Mwanadada huyo alikuwa anafurahia kumshika paka wake karibu na shavu kabla ya kugundua paka alikuwa na panya mdomoni.

Muhtasari

• Baada ya kugundua paka wake alikuwa na panya mkubwa mdomoni, mwanamke huyo alimrusha chini na kukimbia akilia.

Binadamu wengi wanapenda sana kufuga Wanyama kama mbwa na paka kama marafiki wao wa nyumbani.

Kuna mwanamke mmoja ambaye alichukua paka wake na kumbeba karibu na shavu lake akichukua klipu kumbe yule paka alikuwa na panya mdomoni.

Klipu ya jinsi mwanamke huyo alijibu baada ya kugundua paka alikuwa na panya mdomoni imezuzua wanamitandao, kwa jinsi alivyomrusha yule paka chini na kukimbia kwa kasi mno.

Video hiyo ambayo ilipakiwa TikTok na kusambazwa pakubwa mpaka kwenye Twitter iliwaacha wengi wakicheka, haswa jinsi yule mwanamke alikuwa na furaha kumbeba paka wake kuchukua video karibu na shavu lake la kulia.

Kwenye kamera ndio aliona mdomoni mwa paka kulikuwepo na panya ambaye paka yule alikuwa hataki kabisa kumuachilia.

“Sijamaliza kucheka kwa tukio hili, nimechoka. Sikuwa najua huyu paka alikuwa na panya mdomoni,” mwanadada huyo alilia.

“Nimefurahiya sana hii iliwapa kila mtu kicheko sawa na ilivyonichekesha,” mwenye kupakia klipu hiyo aliandika.

“Maono yake ya pembeni yaliingia wakati huu hasa kwa nini mimi si paka,” mwingine alitania.