Hii sio haki, nabeba mtoto tumboi miezi 9 anakuja kufanana babake! - Mama ateta (+video)

Mama huyo alisema anahitaji kufidiwa uharibifu wa kihisia kutokana na kitendo cha mtoto kufanana babake.

Muhtasari

• “Hii sio haki 😩 wanahitaji kunilipa kwa uharibifu wa kihisia,” aliongeza.

Mwanamke mmoja kwenye mtandao wa TikTok amewashangaza wengi baada ya kulalama vikali ila tu kwa utani kuhusu mtoto wake kutomfanana.

Mwanamke huyo katika klipu hiyo ya Tiktok alisema kwamba mtoto wake hakumfanana kama alivyokuwa akitarajia bali alifanana babake.

Alilalama kwamba hiyo ilikuwa kama hujuma kutoka kwa mtoto wake baada ya kumbeba kwa zaidi ya wiki 40 na siku kadhaa za ushee.

Mama huyo mpya, aliyetambuliwa kwenye TikTok kama Stephny Ike, alisema mtoto wake, ambaye alitumia miezi tisa tumboni mwake, alitoka akifanana na mumewe. Katika video ya TikTok, Stephny alisema anapaswa kulipwa kwa uharibifu wa kihisia ambao amepitia.

Wengi baada ya kuona picha hizo, walielewa utani wake na kuendeleza utani huo kwa kusema jinsi watoto kufanana mama au baba kuna faida zake na wengine kusema haijalishi.

“Nilikubeba kwa miezi tisa ndio uje kutokea kufanana kabisa na babako. Alinifanyia ubadhilifu baada kumbeba kwa wiki 40 na siku tano juu,” Stephny aliandika kwenye video hiyo na pia kuifuatia kwa sauti ya maneno hayo.

“Hii sio haki 😩 wanahitaji kunilipa kwa uharibifu wa kihisia,” aliongeza.

Katika picha ya pamoja na kitoto hicho na babake, mtu kwa kutazama mara moja tu unaweza ukakubaliana naye kwamba ni moja kwa moja mfanano wa baba mtu.

Wengine waliandika kwamba kama ni mtoto wa kike ni sawa kwani inatarajiwa hivo kuwa watoto wa kike aghalabu huchukua sura na tabia za baba huku wa kiume wakichukua sura za mama zao.