"Photocopy ya Mulamwah!" Watu wacharuka kwenye picha ya Carrol Sonie na bintiye

Sonie alidokeza kwamba wiki hii ndio mwanawe anafikisha mwaka mmoja.

Muhtasari

• “Huyu ni nakala ya Mulamwa, sijui kwa nini tudem hukaa baba zao,” shabiki wake aliandika.

Sonie kwa mara ya kwanza aonesha sura ya mwanao na Mulamwah aliyekuwa mkubwa
Sonie kwa mara ya kwanza aonesha sura ya mwanao na Mulamwah aliyekuwa mkubwa
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza tangu kutengana na Mulamwah, mwigizaji Carrol Muthoni almaarufu Sonie ameonesha picha ya mwanao, Keila ambaye wiki hii anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Kupitia Instagram yake, Carrol Sonie alipakia picha yake akiwa ameshika uzao wat umbo lake mikononi katika picha moja maridadi kabisa ambayo imezua bashasha mitandaoni.

Baadhi hawakukosa kufanya udadisi wao kuhusu sura ya mtoto, haswa baada ya madai mengi kuzunguka kuvunjika kwa mahusiano yao ni kutokana na mtoto huyo kutokuwa mwa mchekeshaji Mulamwah.

Katika picha hiyo mpya, wengi walisema mtoto huyo ni chapisho kamili la Mulamwah na hata wengine kuzua dhana kwamba watoto wa kike aghalabu huchukua sura za baba zao.

“Ikiwa kufura alikuwa mtu, ushindi ungeenda moja kwa moja kwa Keila😂😂🤦🏾‍♀️ Hata hivyo, ni wiki yake ya kuzaliwa,” Carrol Sonie aliandika.

“Huyu ni nakala ya Mulamwa, sijui kwa nini tudem hukaa baba zao,” shabiki wake mmoja kwa jina Shan Hairpalour alindika.

Sonie mapema wiki jana pia alizikata dredi zake za muda mrefu ambapo kwa sasa ana muonekano mpya. Alipokuwa akinyoa, alisema kwamab aichukua uamuzi huo ili kuona kama mambo mapya na mazuri yatamfuata.

Mulamwah na Sonie walitengana mwishoni mwa mwaka jana katika kile kilichofuatia kutupiana maneno makavu kweney mitandao ya kijamii  na katika mahojiano na wanablogu.