(+video) "Nimenyoa nione kama mambo yataenda sawa" - Carrol Sonie asema akinyoa dredi

Katika sanaa yake ya uigizaji, dredi hizo zilikuwa kama utambulisho wake kwa muda mrefu

Muhtasari

• “Tumenyoa tuone Kama mambo yataenda Sawa” Muthoni alisema kwenye Instagram.

• Sonie sasa anajiunga kwenye orodha ndefu ya watu mashuhuri walionyoa dredi zao, japo kundi hili ni la wanaume

Muigizaji Carrol Muthoni Sonie hatimaye amenyoa dredi zake ambazo kwa muda mrefu zilikuwa kama utambulisho wake.

Katika video ambayo Muthoni aliipakia kwenye Instagram yake, alionekana ameketi kweney kinyozi akikatwa rasta moja baada ya nyingine huku akidokeza kwamba ameamua kuchukua hatua hiyo ili kuona kama mambo yatabadilika.

“Tumenyoa tuone Kama mambo yataenda Sawa” Muthoni alisema kwenye Instagram.

Kwa muda, Muthoni amekuwa akigonga vichwa vya habari haswa tangu ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake na ambaye pia ni mzazi mwenzake, Mulamwah baada ya wawili hao kutupiana maneno yasiyoandikika kwa wino wowote.

Mwezi mmoja uliopita, Muthoni alirudi tena kwenye mwanga baada ya kufichua kwamab amewahi mpenzi mpya.

Ila tamko hili halikupokelewa vizuri na Mulamwah aliyeenda mbele na kuachia maneno mengi ya kashfa akiyaambatanisha na picha alizokuwa akidai kwamba Sonie ameendea mwanaume ambaye anamzidi kiumri mara dufu.

Mulamwah alifichua kwamba mpenzi ambaye Sonie alikataa kufichua sura yake hakuwa kijana kama yeye bali ni mtu rika la baba yake, jambo ambalo Sonie alilibisha kwa kusema kwamba anachojua yeye ni kwamba mchumba wake hajamwaacha mbali sana kiumri.

Alizidi kujitetea kwamba mwanaume Mulamwah alikuwa akizungumzia ni mhubiri ambaye alikuwa anamsaidia katika maombi wakati Sakata la kuachana lilikuwa linamuumiza kichwa na mpaka kumfanya kutofikiria kisawasawa.

Kauli yake kwamab amenyoa ili aone kama mambo yatabadilika imechukuliwa na wambea wa udaku na kutafsiriwa kwa njia tofauti.

Sonie sasa anajiunga kwenye orodha ndefu ya watu mashuhuri walionyoa dredi zao, japo kundi hili ni la wanaume, Sonie anakuwa mwanamke wa kwanza kujinafasi kwenye orodha hiyo.

Thee Pluto, Sean Andrew, Timmy Tdat, Magix Enga, Willis Raburu ni miongoni mwa watu mashuhuri walioweka wazi kunyoa rasta.