Kamati ya roho chafu! Shabiki atabiri Pozee na Jovial kutengana kabla ya Desemba (+screenshot)

Shabiki huyo alimfokea kuwa hawatafika Desemba kama hawajaachana

Muhtasari

• “Pozee kwani mlikuwa kweli, wewe ni mwanaume ambaye unahakikisha ahadi yako imetimia, ulituambia tu mwezi jana,” Chriswin alikumbuka.

Shabiki asuta mahusiano ya Willy Paul na Jovial
Shabiki asuta mahusiano ya Willy Paul na Jovial
Image: Instagram

Msanii Willy Paul wikendi iliyopita alikuwa gumzo kubwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya msanii wa kike Jovial kudokeza kwenye Instastories zake kuwa huenda wamezama katika mapenzi na mkurugenzi mkuu huyo wa lebo ya Saldido International.

Fununu za wawili hao kuwa katika mapenzi zilianza takribani mwezi mmoja na ushee hivi uliopita ambapo Pozee alianza kuandika jumbe kwenye mitandao yake ya kijamii akionekana kumrushia mistari Jovial.

Ghafla suala hilo lilitulia na Jovial safari hii ndiye aliyeliibua kwa kupakia picha ya Pozee na kusema kwamba anahisi kabisa amezama kwenye mapenzi.

Pozee alifanya kweli kwa kupakia video kwenye Instagram yake akiwa anamkaribisha Jovial kutoka ziara moja.

Katika video hiyo, Pozee anaonekana akimkumbatia Jovial na kumpandisha ndani ya gari lake alilolizindua wiki jana kabla ya wawili hao kufunga mlango na kuamrisha dereva kuendesha kuwapeleka sehemu ambayo waliijua wenyewe.

Video hiyo iliashiria wawili hao kuwa na chembechembe za huba baina yao, jambo ambalo wengine walisema kuwa huenda ni kiki ya ngoma ambayo wanatarajia kuachia hivi karibuni kama collabo.

Wengine ambao ni wanachama katika kamati ya roho chafu walimkejeli kando na matatu yake pia hata mahusiano yake na Jovial waliyapiga mafamba kwa kusema kwamba wataachana tu muda si mrefu.

Katika mtadandao wa Insta, Pozee na Jovial waliona siku mrefu ambapo watumizi wa mtandao uo waliwatamkia maneno ya kila aina na mzomo wa kila rangi.

“Pozee anaenda kuegesha hili gari kwa kitanda,” Addifela aliandika.

“Desemba haifiki kama hamjaachana,” mwingine kwa jina Steve aliyatupia dongo mahusiano ya wasanii hao wawili.

“Pozee kwani mlikuwa kweli, wewe ni mwanaume ambaye unahakikisha ahadi yako imetimia, ulituambia tu mwezi jana,” Chriswin alikumbuka.

Ikiwa wawili hao wataoana basi wataingia katika vitabu vya historia ya wasanii wa muziki ambao waliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na hata kufunga ndoa wakiongozwa na Nameless na mkewe Wahu, Arrow Bwoy na mpenzi wake Nadia Mukami miongoni mwa wengine.