Ajuza wa miaka 70 ataka mwanamume wa kumuoa kabla hajafa

Niko tayari kuwa mke na kuhamia pamoja na mpendwa wa maisha yangu - Alphonsine Tawara.

Muhtasari

• Tawara alikiri kwamba anatarajia kupenda na kufurahia matunda ya ndoa kabla hajafariki.

• Mwanamke huyu alifichua kuwa alijitolea maisha yake kuwasomesha ndugu zake na kuwafukuza wanaume waliomwomba mkono wa ndoa miaka yake ya ujana.

Ajuza asema anatafuta mume mwenye upendo atakae muoa kabla hajafa
Ajuza asema anatafuta mume mwenye upendo atakae muoa kabla hajafa

Ajuza wa miaka 70 alizua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusikika akisema anatafuta mume mwenye upendo atakayemuoa kabla hajafa.

Mwanamke huyu alikuwa anazungumza kwenye mahojiano na chaneli moja ya YouTube ambapo alidai bado ni bikira na azimio lake kuu ni kupata mchumba.

Kulingana na nyanya huyu anayejulikana kama Alphonsine Tawara, alikiri kwamba anatarajia kupenda na kufurahia matunda ya ndoa kabla hajafariki.

Mwanamke huyu alifichua kuwa alijitolea maisha yake kuwasomesha ndugu zake na kuwafukuza wanaume waliomwomba mkono wa ndoa miaka yake ya ujana.

"Nikipata mume, ninaolewa. Niko tayari kuwa mke na kuhamia pamoja na mpendwa wa maisha yangu," alisema.

Tawara na anayeishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alisema yuko tayari kutulia ikiwa atapata mwanamume mwenye upendo wa kukaa naye maisha yake yote.

Mbali na hayo bikizee huyu aliwashaangaza wengi ambapo alipodai anataka mwanamume ambaye si mvivu.

Ajuza huyu alisema yuko tayari kutulia ikiwa atapata mwanamume mwenye upendo wa kukaa naye maisha yake yote.

Licha ya hayo ajuza huyu alisema hana mtoto wa kumzaa ila ni mama wa watoto wengi kwa sababu yeye ni mwalimu ambaye amekuwa akitoa huduma za masomo kwa wanafunzi tangu alipohitimu.