Murife Run!Mbunge Salasya aambiwa baada ya Manzi wa Kibera kuomba amuoe

Savula amemwambia Salasya kwamba jambo bora zaidi kufanya sasa ni kuiga Murife run kwa kukimbilia maisha yake ya baadaye.

Muhtasari
  • Manzi Wa kibera anayefahamika kwa tabia yake ya kutafuta kiki aliandamana zaidi na nambari yake ya simu ya kibinafsi chini ya bango hilo
Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya Salasya afichua sifa za mwanamke ambaye anamtafuta
Peter Salasya Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya Salasya afichua sifa za mwanamke ambaye anamtafuta
Image: Facebook

Mbunge Peter Salasya ameonywa dhidi ya kukubali ndoa na mwanasosholaiti mmoja maarufu Manzi Wa Kibera.

Hii ni baada ya mwanasosholaiti huyo ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akijiweka hadharani kuingia katika mitaa ya jiji la Nairobi akiwa amebeba bango lililoandikwa kwa herufi kubwa 'Marry Me Peter Salasya, Manzi Wa Kibera'.

Manzi Wa kibera anayefahamika kwa tabia yake ya kutafuta kiki aliandamana zaidi na nambari yake ya simu ya kibinafsi chini ya bango hilo, akionyesha ujasiri wake wa hali ya juu na dhamira ya kuolewa na mbunge huyo.

Akitoa hisia zake kuhusu ili naibu Gavana wa Kakamega Mhe Ayub Savula ambaye alikumbana na chapisho hilo baada ya kusambaa kwa mitandao ya kijamii alimuonya  mwenzake, Mbunge Salasya kuhusu dhiki inayokuja.

Alidai kuwa mwanasosholaiti huyo amekuwa katika ndoa lakini aliachwa hivi majuzi na hatua yake ya kumkaribia ni lazima iwe ya samaki.

Wakati huo huo, Savula amemwambia Salasya kwamba jambo bora zaidi kufanya sasa ni kuiga  Murife run kwa kukimbilia maisha yake ya baadaye.

"Mwanangu Peter Salasya! Usiseme Ayub Savula hakukuonya! Kama huyu anayeitwa Manzi Wa Kibira ni mwanasosholaiti ambaye hata alifunga ndoa hivi majuzi. Sasa ameachwa na anakutaka  wewe. Mwanangu uwe kama Murife. Kimbia! SALASYA KIMBIA. @P_Salasya," Aliandika Ayub.

Ombi la Manzi wa Kibera lilijiri siku moja baada ya mwanasiasa huyo kukutana na mwanadada aliyeomba awe mke wake.