(+video) Mwanaume agoma kununua chakula baada ya mpenziwe kuwasili na rafiki

Inadaiwa mwanamke alikuwa ameonywa asikuje na mtu mwingine mgahawani ila yeye akaja na mwanadada rafiki yake.

Muhtasari

โ€ข Kulingana na mwanamume huyo alisema chakula ambacho angemudu kununua kilikuwa chake na mpenzi wake pekee.

Image: Tiktok

Mwanamume mmoja aliwashangaza sana watumizi wa mitandao baada ya kuonekana kwenye video akikataa katakata kumnunulia chakula rafiki wa mpenzi wake aliyekuja naye kwenye ''Date''

Inaaminika mwanamume alikuwa amemwalika mpenzi wake mgahawani washiriki chakula pamoja ila mpenzi wake akaja na mwanadada rafiki yake.

Mwanamume huyo alisema chakula ambacho angemudu kununua kilikuwa chake na mpenzi wake pekee

Video hiyo iliyosaamba kwenye mtandao wa Tiktok iliwafanya walioiona kumdhihaki mwanamke ambaye hakupewa chakula siku hiyo.

Katika klipu hiyo, mwanamume kwenye ''Date'' yao na mpenzi wake walionekana kufurahia mlo huo, bila kusumbuliwa na mtu mwingine kwenye meza yao huku mwanamke aliyejiongeza akionekana kusononeka.

Rafiki ya mwanamke huyo alionekana akiwa ameketi huku mikono yake ikiwa mapajani mwake akitazama bila kutamka lolote.

Ila watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walimrushia cheche za matusi mwanadada huyo kwa kumruhusu rafiki yake kuaibishwa kwa njia hiyo, huku wanaume wakimpongeza mwanamume huyo kwa kumpuuza mwanadada aliyejiongeza.

 "Hapana hata kama mwanamume atanunua chakula basi wangegawana na rafiki yake." Jamaa mmoja alisema

"Wanaume!, Jamaa  amefanya ile kitu ya Brotherhood... Wanaume tunahitaji kuwa na mkutano...Mtu huyu anahitaji kupandishwa cheo mara moja." mwingine alimpongeza mwanamume huyu.

''Mwanamke anayejitegemea anaweza hata kulipa'' mwanadada mtumizi wa mitandao alitoa kauli yake.