Amber Ray kavishwa pete ya uchumba?

Vilevile, Rapudo alizidi kueleza matukio yaliyomtokea baada ya Amber Ray kumbwaga mwezi mmoja uliopita.

Muhtasari
  • Amber ni mpenzi wake Rapudo ambaye waliachana  na kurudiana tena wiki 3 ziliopita
Amber Ray na Rapudo kwenye Mtoko huko Lamu
Image: RAPUDO//INSTAGRAM

Mwanasosholaiti maarufu nchini Faith Makau almaarufu kama Amber Ray yuko kwenye mahaba ya upendo.

Amber ni mpenzi wake Rapudo ambaye waiachana  na kurudiana tena wiki 3 ziliopita.

Rapudo alichapisha picha kwenye mtandao wake wa Instagram  iliyoandikwa:

'Mwisho wa siku nitarudi kwako nikikimbia, si kwa sababu mimi ni mnyonge bali ni kwa sababu nilizama katika bahari ya mapenzi na wewe, siwezi kuwa bandia kuigiza kuwa mgumu, hiyo ni ya watu wapweke," Rapudo aliandika kwenye Insta story yake.

Vilevile, Rapudo alizidi kueleza matukio yaliyomtokea baada ya Amber Ray kumbwaga mwezi mmoja uliopita.

Alieleza kuwa kwa wakati mmoja alijaribu kuwa nunda ila maji yakazidi unga mambo yalipomkaba hadi kwenye koo mpaka kushindwa kufanya mishe za kila siku. Aliongeza kuwa Ray ndiye kitu bora zaidi kichowahi tokea katika maisha yake.

"Nilijaribu kujifanya mgumu lakini naweza sema ukweli wakati ulipoondoka ulienda na kila kitu kizuri kilichokuwa ndani yangu, kitu kizuri ambacho kiliwahi nitokea maishani mwangu," Rapudo alitema nyongo.

Baada ya wawili hao kurudiana,Amber amechapisha picha akiwa Nyanza, ila wengi walidokeza kwamba mwanasosholaiti huyo ameenda kutambulishwa kwa wazazi wa Rapudo.

Huenda ikawa ni kweli, kwani dada yake Amber Ellah Ray amepakia video kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika;

"Hongera Amber Ray na Kennedy Rapudo Mungu abariki muungano wenu,nimepata ndugu leo,"Aliandika  Ellah.

Haya basi wacha tusubiri kama wenzi hao watatngaza habari njema kwa mashabiki.