Eric Omondi ampoteza mwanawe,amuomboleza kwa ujumbe wenye hisia

Eric Omondi alinukuu kuwa usiku wa jana ulikuwa mojawapo ya usiku mrefu zaidi maishani mwake.

Muhtasari
  • Eric Omondi ampoteza mwanawe,amuomboleza kwa ujumbe wenye hisia
  • Alisema hawakuwahi kukutana lakini watampenda milele

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua kwamba mpenzi wake Lynne alipoteza ujauzito wake usiku wa kuamkia leo.

Kwenye chapisho la hisia na mchekeshaji mtata Eric ameomboleza mtoto wao akisema kwamba walijitolea kwa zaidi ya masaa 5 lakini Mungu alikuwa na mipango mingine.

Katika video hiyo tulimwona Lynne akihangaika na anaonekana kuwa na maumivu. Eric Omondi pia anaonekana kujaribu kumfariji.

Eric Omondi alinukuu kuwa usiku wa jana ulikuwa mojawapo ya usiku mrefu zaidi maishani mwake.

Alisema hawakuwahi kukutana lakini watampenda milele.

"Usiku wa jana ulikuwa mojawapo ya usiku mrefu zaidi maishani mwangu. Tulipigana kwa zaidi ya saa 5 kujaribu kuokoa malaika wetu mdogo lakini Mungu alikuwa na mipango mingine. Hatukuwahi kukutana lakini hakika tulikuhisi na tutakupenda milele. Heshima kwa wanawake wote hakuna mwanaume duniani mwenye nguvu za aina hiyo @lynne stay strong it is well."