'Kulia ni afya,'Mashabiki wamfariji Wema Sepetu baada ya kupakia video akilia

Kwenye video hiyo alinukuu akisema kuwa anajua wasichana wakubwa hawalii lakini wenye nguvu ndio hulia.

Muhtasari
  • Daima amejitokeza kujipigania kwa kuwaibu ipasavyo wanaomshambulia
  • Hata hivyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amevunja mioyo ya watu wengi baada ya kusambaza video yake akilia bila kujizuia na kumwaga machozi mengi

Wema Sepetu ni mwanasosholaiti na mwanamitindo kutoka Tanzania . Aliwahi kuwa miss Tanzania 2006 ambapo alipata umaarufu wake.

Baadaye alianza kuchumbiana na diamond Platinumz ambaye wakati huo alikuwa anaanza kazi yake ya muziki na wakaachana huku Diamond akiendelea kuchumbiana na Zari.

Wema pia ndiye mtu mashuhuri wa kike anayefuatwa zaidi Afrika Mashariki.

Wema Sepetu amependwa na watu wengi kwa ujasiri wake na ustahimilivu wake kutokana na mashambulizi ya mitandaoni.

Daima amejitokeza kujipigania kwa kuwaibu ipasavyo wanaomshambulia.

Hata hivyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amevunja mioyo ya watu wengi baada ya kusambaza video yake akilia bila kujizuia na kumwaga machozi mengi.

Kwenye video hiyo alinukuu akisema kuwa anajua wasichana wakubwa hawalii lakini wenye nguvu ndio hulia.

Chapisho hilo limewafanya mashabiki wake wengi kumuhurumia kwani walisema inawaumiza akilia.

Wengine pia wamemwambia kwamba kila kitu anachopambana nacho kitakuwa sawa na anapaswa kuendelea kuomba.

Hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

sharonmining89A : see only your beautiful eyes my darling @wemasepetu

shamsaford: @wemasepetu 😭😭 kulia ni afya bby

dayon_samy: Wema wewe najua kinachokutesa ni kupata mtoto nakuambia hakuna kitu kinashndikana kwa mungu watu wanazaa mpaka uzeeni na nikwambie sio kila mwenye watoto anafuraha hapana wapo watu wamezaa lakin ni kama hawajazaa wengine wanapigwa mpka na watoto wao na kujuta bora asingezaa niamini wanadamu hatutosheki

jo_wonder1: Usipende kuwalaumu watu unaodhani wanaweza kukusaidia labda ni marafiki zako au ni ndugu zako au ni watu unaowaamini sana na kuwategemea. Sikia USIWALAUMU bali uwashukuru maana ilikuwa lazima