Pritty Vishy azungumza baada ya kuonekana akimbusu tiktoker mwanamke

Vishy pia anaonekana akimuinua juu tiktoker huyo huku wakicheza densi.

Muhtasari

•Hivi majuzi, wawili hao walifurahiya muda pamoja na kuchapisha baadhi ya matukio kwenye kurasa zao za Instagram.

•Pritty amewahi kubainisha mara kadhaa alikuwa ameonywa kuhusu TikToker.

Pritty Vishy
Image: INSTGRAM// PRITTY VISHY

Aliyekuwa mpenzi wa mwimbaji maarufu Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akijivinjari na TikToker Becky Akinyi kwa njia ya kimahaba.

Hivi majuzi, wawili hao walifurahiya muda pamoja na kuchapisha baadhi ya matukio kwenye kurasa zao za Instagram.

Marafiki hao pia walishirikisha mashabiki wao katika kipindi cha moja kwa moja ambapo walionekana wakibusu mara kadhaa kwenye midomo huku wakibugia vinywaji. Wawili hao walionekana kuwa kwenye klabu.

Katika video ambazo zimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, Vishy pia anaonekana akimuinua juu tiktoker huyo huku wakicheza densi.

Wanamitandao ambao walitoa maoni chini ya video ambayo wawili hao walichapisha waliibua maswali mengi wakitaka kufahamu uhalisi wa uhasiano wao.

Vishy na Becky wamekuwa marafiki kwa muda mrefu na mara nyingi wawili hao wamekuwa wakikutana na kufurahia muda pamoja. Kufuatia tukio la hivi majuzi, tetesi zimeibuka kuwa huenda wanachumbiana.

Pritty amewahi kubainisha mara kadhaa alikuwa ameonywa kuhusu TikToker.

Mpenzi huyo wa zamani wa Stivo Simple Boy hata hivyo aliweka wazi kuwa alimpenda Becky na kwamba urafiki wao hautaisha hivi karibuni.

Siku ya Jumatatu, Pritty alivunja kimya kuhusu unyanyasaji wa mtandaoni huku akidai kwamba amekuwa akikejeliwa kwa sababu ya umbo lake la mwili.

Mtumbuizaji huyo alibainisha kuwa anatamani angekuwa kuwa na umbo tofauti wa mwili ili aweze kupendwa.

"Je, nilimwomba Mungu aniumbe hivi? Hapana. Sikufanya hivyo, ikiwa ningechagua jinsi nitakavyozaliwa, ningetaka kufanana na Beyonce na Nicki Minaj." alisema.

"Kupitia unyanyasaji kutoka kwa watu wanaopaswa kukushikilia, kuonewa mitandaoni na kukataliwa sio rahisi, wakati mwingine natamani kupendwa hata na wachache tu lakini nani atanipenda?"

"Kibaya zaidi ni kukosa mtu ambaye atakushika, atakupa moyo na nguvu ..Hata kukumbatiwa ili kupunguza maumivu na huzuni," alisema.

Image: HISANI