Whozu kubadilisha dini kuwa Muislamu kabla ya kufunga ndoa na Wema Sepetu

"Nitasilimu na kufunga ndoa naye mwaka huu," alisema.

Muhtasari

•Mwanamuziki Whozu atabadilisha dini kuwa Muislamu kabla ya harusi yake na Wema Sepetu baadaye mwaka huu.

•Wema aliwaambia wenye shaka kuwa yuko kwenye mapenzi sana.

Wema Sepetu na Whozu

Mpenzi wa muigizaji wa Bongo Wema Sepetu Whozu atabadilisha dini kuwa Muislamu kabla ya harusi yao baadaye mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo  moja cha redio nchini Tanzania, Whozu alisema hakuna kitakachomzuia kufunga ndoa na Wema.

"Nitasilimu na kufunga ndoa naye mwaka huu," alisema.

Wema na Whozu wamekuwa marafiki wakubwa kwa muda mrefu kabla ya kutangaza ndoa yao mwaka jana, 2022.

Wema aliwaambia wenye shaka kuwa yuko kwenye mapenzi sana.

"Wacha wanaochukia wachukie. Upendo ni mzuri. Hujui maana ya upendo kwa sababu haujapendwa."

Aliongeza kuwa sasa ana furaha kutokana na mpenzi wake mpya.

"Kilicho muhimu ni furaha yangu. Furaha yangu huja kwanza na mengine yanafuata."

Mwaka jana, wanandoa hao walipoteza ujauzito wa miezi mitatu.