Mume avunja ndoa ya miaka 20 kwa sababu mkewe ana tabia ya kupakulia majirani chakula

Mume huyo aliiambia mahakama kuwa mkewe ana mazoea ya kugawa chakula chao kwa majirani na watoto wao licha ya uchumi kuwa mbaya.

Muhtasari

• Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi Harriet Mulenga, alibainisha kuwa sababu za kuachana kwa wanandoa hao hazina msingi.

• Lakini kwa sababu mlalamikaji alisisitiza kwamba hataki mke wake, mahakama ilikubali talaka.

Image: MARGARET WANJIRU

Mwanamume mmoja nchini Zambia amewaacha watu kwa mshangao kubwa baada ya kumpa mkewe talaka kwa sababu ya kuwa na mazoea ya kuwapakulia majirani chakula.

George Phiri mwenye umri wa miaka 49 aliamua kumuacha mkewe Tanta Zulu mwenye umri wa miaka 34 ambaye walidumu naye kwa ndoa ya miaka 20, tovuti ya Zambian Observer iliripoti.

Phiri aliamua kumshtaki mkewe mwishoni mwa juma katika mahakama ya Matero, akidai anatabia ya kugawa chakula, akiongeza kuwa amekua akiwapatia na watoto wa hao majirani.

Akijitetea, Zulu aliiambia mahakama kuwa mumewe alikuwa ni bahili na mkali hadi anafikia hatua ya kupima chakula kilichopo ndani ya nyumba kabla ya kwenda kazini, tovuti hiyo ilisema.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi Harriet Mulenga, alibainisha kuwa sababu za kuachana kwa wanandoa hao hazina msingi.

Lakini kwa sababu mlalamikaji alisisitiza kwamba hataki mke wake, mahakama ilikubali talaka.

 

Itakumbukwa tena nchini humo miezi kadhaa nyuma mwanamke mmoja alishangaza mahakama baada ya kudai kuwa alitaka kumuacha mumewe kwa sababu ya kumpata amenyoa sehemu nyeti bila kumtaarifu.

Katika taarifa hiyo ya kushangaza ambayo ilichapishwa na vyombo vya habari nchini humo, mwanamke huyo alisema kuwa alikuwa anataka talaka kwa sababu aligundua mumewe ana mwanamke wa pili na yeye hangeweza kuvumilia ndoa ya wake wawili.

Akiulizwa alijuaje kuwa mumewe ana mke wa pili, mwanamke huyo kwa jina Karen Chungu alisema kuwa siku moja alitaka kufanya mapenzi na mumewe lakini akapigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa alikuwa amenyoa nywele za sehemu za siri.