Mchekeshaji Nasra Yusuf ametangaza kuwa rasmi kuwa milionea

"Najitolea kutoa pia 15% ushuru wa kidijitali ya mdosi wenu," Nasra aliandika.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo alidai kuwa kufikia sasa jambo linalomridhisha zaidi ni kulipwa katika sarafu ya dola.

Nasra Yusuf ajitangaza kuwa Milionea
Nasra Yusuf Nasra Yusuf ajitangaza kuwa Milionea
Image: Instagram

Mchekeshaji Nasra Yusuf ametangaza kuwa yeye ni milionea sasa.

Nasra alielezea kwenye Instastories zake  kwamba alikuwa na hofu ya kutimiza umri wa miaka 30 mwezi Oktoba bila kuwa na milioni katika akaunti yake.

"Wakati fulani siwezi kuamini kwamba tuko mwezi wa Juni, nadhani maombi niliyopata kutoka kwa wakazi wa Wajir yanafanya kazi," aliandika Nasra kwenye Instastory yake.

Nasra alisema ni Mungu tu aliyefanikisha ndoto yake. Pia aliongeza kwa kusema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ameifanikisha ndoto yake ya kuwa milionea miezi 3 kabla ya kutimiza umri wa miaka 30.

Mchekeshaji huyo alidai kuwa kufikia sasa jambo linalomridhisha zaidi ni kulipwa kwa dola.

"Naona niweke ka party walahi #MillionareNasra," Nasra aliandika kwa mbwembwe.

Mchekeshaji huyo aliendelea na kuandika,"nikikushauri unaniskiza."

"Najitolea kutoa pia 15% ushuru wa kidijitali ya mdosi wenu," Nasra aliandika kwa mbwembwe.

Nasra aliendelea kwa kuwaambia wanaomuomba pesa wangoje kwanza hataki ipungue na kuwa hadi yeye saa hii anajinyima.

Siku iliyopita pia wajasiriamali Simon Kabu na mke wake Sarah Kabu wametangaza kuwa wao ni mabilionea rasmi.

Wanandoa hao wanaomiliki kampuni ya usafiri ya Bonfire Adventures wakizungumza kwenye mahojiano na Youtuber wa Ghana Wode Maya, walifichua kuwa sasa wameingia kwenye kikundi cha mabilionea.

"Tunamshukuru Mungu kwa kuwa sasa sisi ni mabilionea. Kampuni yetu sasa ina dhamani ya zaidi ya bilioni " Sarah Kabu alisema.