Simulizi: Kijana wa miaka 27 achizishwa na mahaba ya ajuza wa miaka 60, wapanga ndoa

Ajuza huyo aliweka wazi kuwa mpenzi wake akimuacha atakufa

Muhtasari

• Ajuza huyo alikiri penzi lake la dhati kwa mpenzi huyo wake baro baro ambaye amechumbiana  naye kwa muda wa miaka mitatu baada ya mume wake wa awali kuaga dunia.

• Lucas lisema kuwa licha ya kejeli kutoka kwa majirani wakati walipoanza mahusiano hayo, yeye alihisi hawafai kukejeliwa kwa kuwa mapenzi hayatambui umri.

Kijana wa miaka 27 akimbusu bibi wa miaka 60.
Kijana wa miaka 27 akimbusu bibi wa miaka 60.
Image: SCREENGRAB/MBENGO TV

Mjane mmoja nchini Tanzania amefichua kuwa anapanga kufanya ndoa na mpenzi wake wa miaka mitatu, kijana wa miaka 27.

Katika mahojiano na Mbengo TV, Ajuza huyo mwenye umri wa miaka 60 alikiri penzi lake la dhati kwa mpenzi huyo wake baro baro ambaye amechumbiana  naye kwa muda wa miaka mitatu baada ya mume wake wa awali kuaga dunia.

Mwanamke huyo anyefahamika kama Eustah Lucas alisema kuwa yeye ndiye aliyeanza kumtongoza kijana huyo na kumuomba kuwa katika mahusiano ya kimapenzi naye.

Mimi ndie nlianza kumteka, mpenzi wangu alikuwa anakuja dukani kukula na ananipata, siku moja nikamkaribisha chakula na akachukua akaenda kula nyumbani.”

Mama huyo wa watoto 6 alisema kuwa licha ya kejeli kutoka kwa majirani wakati walipoanza mahusiano hayo, yeye alihisi hawafai kukejeliwa kwa kuwa mapenzi hayatambui umri.

Kijana huyo anayefahamika kama Shynn alipoulizwa chanzo cha kuvutiwa na mwanamke huyo wa rika moja na mama yake alisema kuwa mama huyo mzee anamjali na kumpenda sana na hii ndiyo chachu ya kumpenda.

Alimsifia mke wake mtarajiwa kuwa ana mahaba na anamjali, kile ambacho kulingana naye hakikuwa rahisi kupata kutoka kwa wasichana wa rika moja naye.

“Alinivutia sana na urembo wake na pia anajali, ma slayqueen wanasumbua na maisha ni mafupi na kwa hivyo sikutaka kuumia na nikamchagua huyu kwa maana ananijali, ananipenda, kila kitu ninachotaka ananinipa”

Mahusiano ya wapenzi hawa wawili yalitiliwa shaka na wafuasi katika mitandao ya kijamii ya Youtube huku wengi wakisema kuwa kijana huyo anataka kuolewa kwa sababu ya mali ya bibi Yule.

Mwanaume huyo aliwakosoa wanaotilia shaka penzi lake kwa Lucas akisema kuwa hakuwa naye kwa sababu ya pesa bali ni kwa sababu bibi huyo alimpa amani ambayo hakupata katika mahusiano na wasichana wadogo kiumri.

“Ndio, aliachiwa mali na mume wake wa awali lakini mimi ninafanya kazi zangu na sitaki pesa zake, kipato changu kidogo lakini sijafuata mali nimefuata penzi na amani ya moyo.”

Nyanya huyo wa wajukuu wanne alipoulizwa kama kuna pingamizi kutoka kwa watoto wake, alifoka na kusema kuwa watoto wake hawana la kusema kuhusiano na maisha yake ya kimapenzi.

“Siogopi chochote maana nimeshapenda, ni rika ya watoto wangu lakini nishapenda, watoto wangu hawezi niambia kitu chochote ni watoto kwangu.”

Bibi huyo pia aliongeza kuwa mpenzi wake akieza tengana naye itamuuma sana na ata inaweza kuwa sababu ya yeye kuaga.

“Akiniacha patachimbika na nampenda sana nitahisi nitakufa kiniacha.” Alizungumza bibi huyo kwa kile kilichoonekana ni kumtishia.