Azziad ajiondoa studioni baada ya kuulilzwa sababu ya kubatilishwa kwa uteuzi wake

Tukio hilo, lililonaswa moja kwa moja wa TikTok, lilizua mjadala mkali kuhusu mipaka ya wanahabari katika juhudi zao za kuweza kuwaharifuu wasikilizaji.

Muhtasari

• Pindi tu mtangazaji huyo alipomuuliza Azziad swali hilo, soshalaiti huyo alisema kuwa swali hilo halikuwa sawa na lilikiuka maelewano yao wa hapo awali.

Azziad Nasenya akiwa katika Ikulu ya Nairobi katika uzinduzi wa Talenta Hela.
Azziad Nasenya Azziad Nasenya akiwa katika Ikulu ya Nairobi katika uzinduzi wa Talenta Hela.
Image: Instagram

Mwanatiktok maarufu, Azziad Nasenya alijiondoa kwenye mahojiano na mtangazaji mmoja wa radio baada ya kuulizwa kuhusu uteuzi wake kwenye baraza la Talanta Hela kubatilishwa.

Pindi tu mtangazaji huyo alipomuuliza Azziad sababu ya uteuzi wake katika baraza hilo, alionekana kukerwa na swali hilo na kuondoka nje ya studio akisema kuwa swali hilo halikuwa sawa na na tayari walikuwa wameelewana hapo awali.

Tukio hilo, lililonaswa moja kwa moja kwa TikTok, lilizua mjadala mkali kuhusu mipaka ya wanahabari katika juhudi zao za kuwaharifuu wasikilizaji.

Aidha mwanahabari huyo alitetea msimamo wake wa kumuuliza swali hilo akisema kuwa ilikuwa wajibu wake kama mwandishi wa habari kuuliza maswali. 

Mtangazaji huyo alidai kuwa swali hilo tata lilikuwa muhimu kwa mahojiano yao kuwa na maana na kutoa habari muhimu kwa wasikilizaji.

Hilo swali si baya, kwa sababu kusema ukweli mimi ni mwanahabari na kama singeuliza swali hilo, mahojiano hayo hayangekuwa na umuhimu wowote kwa wasikilizaji."

Mwanahabari huyo alihisi kuwa kama Azziad hakutaka kuzungumzia swala hilo basi angesema hivyo tu kwa urahisi akiwa hewani kuliko kuondoka katikati ya mahojiano hayo.

Tukio hilo lilibua hisia mseto mitandaoni, wengine walisema kuwa msasa wa Mwende ulikuwa muhimu ili kutoa picha kamili, wengine waliona kuwa mtangazaji huyo alivuka mstari wa faragha na heshima kwa matakwa ya mhojiwa.