Mwanaume ahukumiwa miaka 15 kwa kushika makalio ya jarani wa kike

Kulingana na mwanamke huyo usingizi wake ulikatishwa na mguso wa mwanaume mmoja mwendo wa saa 01:00 usiku na ata kumtambua mwanaume huyo kuwa jirani yake wa karibu.

Muhtasari

• Mwanaume huyo aliamshwa saa saba usiku na mguso kwa makalio yake kwa mtu ambaye hakuwa mume wake. 

• Mwanaume huyo aliisihi mahakama kuomuonea huruma wakati wa hukumu yake akijitetea kuwa alikuwa amelewa chakari.

Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mwanaume mmoja nchini Zambia amehukumiwa kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu kwa kugusa makalio ya jirani yake wa kike wakati mumewe wake hakuwepo.

Mwanaume huyo anayefahamika kama Mathotho anaripotiwa kuingia nyumbani kwa jirani wake mwendo wa saa 01:00 usiku na kuanza kumgusa mwanamke huyo alipokuwa amelala tovuti wa Zambian Observer iliripoti.

Kulingana na rekodi za mahakama, mwanamke huyo alielezea kisa kilicho waacha waliokuwa kwenye mahakama hiyo mdomo wazi.

Kulingana na mwanamke huyo usingizi wake ulikatishwa na mguso wa mwanaume mmoja mwendo wa saa 01:00 usiku na ata kumtambua mwanaume huyo kuwa jirani yake wa karibu.

"Nilipoamka, nilimwona Mathotho akikimbia kutoka chumbani kwangu na nikakimbia kumwamsha babangu," alisema.

Mwanamke huyo alimwelezea baba yake kilichokuwa kimetokea na baba yake akaondoka akiwa amajawa na hasira za mkizi tayari kummaliza Mathotho.

"Nilimjulisha kilichotokea na baba yangu alimfuata Bw Mathotho lakini hakumpata."

Mathotho aliitwa baadaye kwa mkutano katika nyumba ya mwathiriwa lakini akakataa kuhudhuria kwa sababu ambazo alikataa kufichulia mahakama.

Mapuuza ya Mathotho ilimlazimu baba na binti yake kuripoti kesi hiyo kwa Polisi na Mathotho alikamatwa na kuzuiliwa kwa kosa la kumshika visivyo mwanamke huyo.

Mwanamke mke huyo alitakiwa kumtambua mwanaume aliyemdhulumu kimapenzi mahakani, na bila ata kufikiria mara mbili mwanamke huyo almtambua Mathotho.

“Nilimuona aliyenigusa makalio na naweza kumtambua, taa ilikuwa inawaka chumbani. Namjua  Mathotho kwa vile nyumba yake iko karibu na yangu,” alisema kulingana na rekodi za mahakama.

Mwanamke huyo ambaye ni mke ya mwanaume mwingine alisema kuwa mume wake hakuwa nyumbani wakati wa tukio hilo na alihisi ni kama Mathotho alitumia fursa hio kukuja nyumbani kwangu na kujaribu kunidhulumu.

"Nimeolewa lakini mume wangu hakuwa nyumbani na Mathotho alijua kuwa mume wangu hakuwa nyumbani."

Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, Mathotho alikiri kumgusa mwanamke huyo makalio huku mumewe akiwa hayuko nyumbani.

Akihisihi mahakama kuomuonea huruma wakati wa hukumu yake alijitetea kuwa alikuwa amelewa chakari na aliingia nyumba ambayo alikuwa akifikiri ilikuwa kwake na alithani mwanamke huyo alikuwa mke wake. 

Aliambia mahakama kwamba alikuwa amelewa wakati huo na alidhani kuwa ni mke wake kwa sababu nyumba yake iko karibu na yao.

"Kusema kweli, nilikuwa nimelewa na sikujua nilichokuwa nikifanya usiku huo,” Mathotho alisema.

Mathotho alifikishwa mbele ya Jaji wa Mahakama moja nchini Zambia, Mercy Makubalo kwa kuhukumiwa kwa kosa kumdhulumu mwanamke huyo, tukio lililotokea Julai mwaka jana.

Huku akitoa hukumu yake ya miaka 15 ikiambatana na kazi ngumu,Jaji Makubalo alisema kesi za dhuluma za kingono zinaongezeka nchini Zambia na hivyo kunahitajika adhabu kali dhidi ya wakiukaji.