Mastaa wa Kenya ambao wamefanya tafrija ya gender reveal mnamo 2023

Ni njia moja kwa wanandoa kushiriki na marafiki na familia jinsia ya mtoto wao ambaye atazaliwa.

Muhtasari

• Mtangazaji na mwanablogu Presenter Ali na mkewe Medina, waliandaa sherehe ya kifahari ya kufichua jinsia ya mtoto wao.

Sherehe ya dhihirisho ya jinsia ya mtoto
Sherehe ya dhihirisho ya jinsia ya mtoto
Image: Instagram

Sherehe za kudhihirisha jinsia zimekuwa mojawapo ya njia mpya zaidi za kusherehekea ujio wa mtoto.

Ni njia moja kwa wanandoa kushiriki na marafiki na familia jinsia ya mtoto wao ambaye atazaliwa.

Sherehe inaweza kufanywa kutoka wiki 20 baada ya mtu kugundua kuwa ni mjamzito.

Huu ndio muda wa haraka zaidi ambao mtu anaweza kutambua jinsia ya mtoto.

Hapa kuna baadhi ya watu maarufu ambao wamekuwa na sherehe nzuri ya kufichua jinsia ya mtoto:

1. Presenter Ali na Medina Makena

Mtangazaji na mwanablogu Presenter Ali na mkewe Medina, waliandaa sherehe ya kifahari ya kufichua jinsia iliyohudhuriwa na marafiki wa karibu na waundaji wa maudhui.

Wapenzi hao walifurahi kujua kwamba wanatarajia mtoto wa kike.

2. Amber Ray na Kennedy Rapudo

Mwanasosholaiti Amber alitangaza sherehe yake ya dhihirisho ya jinsia kupitia bango ambalo mpenzi wake alitumia maelfu kulitengeneza.

Haikuwa hivyo tu, alifika kwenye tafrija yake kwa chopa.

Wanandoa hao walifurahi kujua kwamba wanatarajia mtoto wa kike.

3. Vera Sidika na Brown Mauzo

Staa wa Reality TV Vera Sidika na msanii Brown Mauzo waliwasili kwa gari la Limousine kwa  tafrija ya kuonyesha jinsia ya mtoto wao wa pili ambaye hajazaliwa.

Ilikuwa katika Hoteli ya Gofu ya Windsor.

Mahali hapo palikuwa pameandaliwa vyema kando ya mto kukiwa na vyakula vingi na champagni za Moet.

Ilidhihirishwa kupitia kwa chopa kwamba wanandoa hao wanatarajia mvulana.

4. Jane Waruguru Kanyi

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu aliyegeuka kuwa mwanasiasa Jane Warunguru ametangaza kuwa anatarajia mtoto wa kike.

Mbunge huyo wa Bunge la Kaunti ya Nairobi alitumia ukurasa wake wa Instagram kushiriki habari hiyo njema na wafuasi wake zaidi ya 58.2k na pia kuangazia matukio machache muhimu kutoka siku hiyo.

5. Naisula Lesuuda

Mbunge wa Samburu Magharibi Naisula Lessuda anatarajia mtoto, na alitangaza tangazo hilo kwa ustadi na picha za kupendeza.

Mwanasiasa huyo anatarajia mtoto wa pili.