Baridi yamuweka Carrol Sonnie katika majaribio ya kumtafuta ex wake

Muigizaji Carrol Sonnie amedokeza kuwa anateseka sana chini ya hali hhi ya hewa ya baridi inayoshuhudiwa kote nchini.

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja alidokeza kuwa hali ya hewa ya sasa inampa mawazo ya kumuita mpenzi wake wa zamani.

•Wapenzi hao  wa zamani walikaribisha mtoto wao wa kwanza wa kike, Keilah Oyando mnamo Septemba 20 mwaka wa 2021.

Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Muigizaji maarufu Caroline Muthoni Ngethe almaarufu Carrol Sonnie amedokeza kuwa anateseka sana chini ya hali hhi ya hewa ya baridi inayoshuhudiwa kote nchini.

Katika taarifa fupi siku ya Jumamosi, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kuwa hali ya hewa ya sasa inampa mawazo ya kumuita mpenzi wake wa zamani.

“Hii weather itafanya ni call ex.. excuses,” Carrol Sonnie aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Threads.

Hata hivyo hakutaja ni yupi kati ya wapenzi wake wa zamani ambaye anajaribiwa kumtafuta ili kusaidiana naye kukabiliana na baridi.

Image: THREADS// CARROL SONNIE

Muigizaji huyo aliachana na mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah mwaka wa 2021, muda mfupi baada ya wawili hao kubarikiwa na mtoto pamoja. Tangu wakati huo wameonyesha uhusiano wao mbaya hadharani mara kadhaa.

Wakati akithibitisha kutengana kwao mwezi Desemba mwaka jana, Sonnie alisema walifanya makubaliano ya pamoja huku akimshukuru baba ya binti wake kwa kipindi cha miaka minne ambacho walikuwa pamoja.

"Hii ni kuweka wazi kuwa mimi na Mulamwah hatuko pamoja tena. Sote tumekubaliana na kuamua kuachana kwa sababu zinazojulikana kwetu. Asante sana kwa upendo na usaidizi mliotupa kwa miaka hiyo 4, mimi binafsi sichukulii kawaida.

Kwa mulamwah, Asante sana kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako kwa miaka hiyo.  Nashukuru sana na nitahifadhi kumbukumbu milele. Katika hatua yako inayofuata maishani, sikutakii kingine ila bora.Endelea kushinda na Mungu akubarikikatika  kila hatua ya maisha yako," Muthoni aliandika.

Wapenzi hao  wa zamani walikaribisha mtoto wao wa kwanza wa kike, Keilah Oyando mnamo Septemba 20 mwaka wa 2021.

Kwa sasa, Carol Sonnie amekuwa akiweka mahusiano yake siri huku mzazi mwenzake Mulamwah akidaiwa kuchumbiana na rafiki yake Ruth K. Licha ya mara nyingi kuonekana wakijivijari pamoja na kuonyesha nyakati za kimahaba, wawili hao wamekuwa wakikanusha kuwa wapenzi.

Mapema mwaka huu, Mulamwah alibainisha kuwa uhusiano wake na 'bestie' wake Ruth K ni wa kirafiki tu.