"Tangu lini polygamy ikawa dhambi" Karen Nyamu ajibu baada ya kushtumiwa kwa kuharibu ndoa ya Samidoh

Seneta Nyamu amejibu baada ya imani yake kutiliwa shaka kutokana na chaguo lake la uhusiano.

Muhtasari

•Shabiki mmoja alimshutumu kuwa mharibifu wa ndoa na kusema kwamba Mungu hawapendi watu kama hao.

•“Nani alisema utaacha kutenda dhambi unapotembea na Yesu. Na tangu lini ndoa ya wake wengi ikawa dhambi," Nyamu alijibu.

Karen Nyamu, Samidoh na Edday Nderitu
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amejibu baada ya imani yake kutiliwa shaka kutokana na chaguo lake la uhusiano.

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa amechapisha picha yake kwenye mtandao wa Instagram na chini yake akafichua jinsi Yesu amekuwa naye katika safari yake ya mafanikio.

"Yesu anatembea naye, hiyo ndiyo nguvu yake kuu," Seneta Nyamu aliandika chini ya picha yake akiwa amevalia sare za skauti.

Katika sehemu ya maoni, shabiki mmoja alimshutumu kuwa mharibifu wa ndoa na kusema kwamba Mungu hawapendi watu kama hao.

“Mungu hapendi mtu anaharibu familia ya wenyewe,” dorcasgift6 alimwambia.

Karen Nyamu ambaye alionekana kutopendezwa na maoni ya mtumiaji huyo wa Instagram alijibu, “Nani alisema utaacha kutenda dhambi unapotembea na Yesu. Na tangu lini ndoa ya wake wengi ikawa dhambi.”

Seneta huyo wa UDA mara nyingi amekuwa akishutumiwa kwa kuharibu ndoa ya mwimbaji wa Mugithi  Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ambaye ana watoto wawili naye.

Katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, wawili hao wanaoaminika kuwa wapenzi wameonekana pamoja sana huku mke wa Samidoh wa miaka mingi, Edday Nderitu akiendelea kufurahia wakati mzuri na familia yake nchini Marekani.

Edday alihamia Marekani ghafla zaidi ya miezi miwili iliyopita lakini hakufichua madhumuni ya ziara yake na muda ambao angetumia katika nchi hiyo iliyo Magharibi mwa dunia.  Pia haijabainika iwapo ndoa yake na mwimbaji huyo wa Mugithi ingali hai.

Mapema mwezi huu, seneta Nyamu alibainisha kuwa ni maombi yake kwamba mpenzi wake Samidoh atakuja kuungana tena na familia yake na Edday Nderitu ambayo imekuwa ikifurahia muda nchini Marekani.

Wakili huyo alithibitisha kuwa ni maombi yake kuwa siku moja Edday atarudi nyumbani ili wawe familia moja kubwa.

Nyamu alikuwa amechapisha nukuu kuhusu kuwasaidia wengine wakati mke huyo wa mzazi mwenzake alipofanywa kuwa mada.

"Kumbuka wakati wowote unapokuwa katika nafasi ya kusaidia mtu, furahiya kufanya hivyo kila wakati kwa sababu huyo ni Mungu anayejibu maombi ya mtu mwingine kupitia wewe," Karen Nyamu aliandika kwenye mtandao wa Facebook siku ya Jumapili.

Shabiki mmoja alijibu, "Siku moja familia ya Edday itaungana tena."

Bila kusita, seneta Nyamu alionekana kukubaliana na maoni ya shabiki huyo na wakati huo akadokeza kwamba angefurahi sana kuona familia ya Muchoki ikiungana na kuwa kubwa tena.

“Ni maombi yetu pia. Tukue familia moja kubwa.”

Katika maoni mengine, shabiki alimuuliza jinsi alivyokuwa akimsaidia mke huyo wa Samidoh kujibu maombi yake.

‘Nashangaa ni maombi gani ya (Edday) ambayo Mungu anajibu kupitia wewe,” Mtumiaji wa Facebook aliuliza.

Karen alijibu, “Mungu atatumia watu wengine kuniamini.