"Ana ndevu, si wa Pwani!" Betty Kyallo afichua maelezo kuhusu mpenzi wake mpya

Betty alifichua kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngozi ya rangi ya chokoleti na ana ndevu.

Muhtasari

•Betty alifunguka maelezo machache ya utambulisho kuhusu mwanamume ambaye anachumbiana naye kwa sasa.

•Mwanahabari huyo pia alibainisha kuwa licha ya kumficha, mpenzi wake ambaye hajatambulika bado anaendelea vyema.

Betty Kyallo
Image: INSTAGRAM

Mwanahabari na mfanyabiashara mashuhuri Betty Kyallo ameapa kuendelea kuficha utambulisho wa mpenzi wake wa sasa.

Katika mahojiano ya simu na kituo kimoja cha redio cha humu nchini, mama huyo wa binti mmoja hata hivyo alifunguka maelezo machache ya utambulisho kuhusu mwanamume ambaye anachumbiana naye kwa sasa.

Betty alifichua kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngozi ya rangi ya chokoleti na ana ndevu. Pia aliweka wazi kuwa mwanamume huyo hajatokea eneo la Pwani.

“Ako tu ni mwanaume. Yeye ni chokoleti ya Ako. Ako na ndevu kiasi chake, sio kama ile injini, lakini kiasi chake. Ako sawa, amebalance. Si wa Mombasa,” Betty Kyallo alisema.

Mwanahabari huyo pia alibainisha kuwa licha ya kumficha, mpenzi wake ambaye hajatambulika bado anaendelea vyema.

“Unataka kumuona ufanye. Acha tu nimfiche hivyo,” alihoji.

Maelezo ya mahusiano ya sasa ya Betty Kyallo yamesalia kitendawili kwa muda wa takriban mwaka mmoja tangu alipotengana na wakili Nick Ndenda. Hata hivyo, mara nyingi amekuwa akidokeza kuwa yuko kwenye mahusiano dhabiti lakini ameweka siri maelezo ya mwanamume ambaye anachumbiana naye.

Mwanahabari huyo alianza kudokeza kwamba amezama kabisa kwenye mahusiano mazito mwishoni mwa mwaka jana.

Mwanzoni mwa mwaka huu,  alifichua kuwa  ana mwanamume ambaye wamekuwa wakichumbiana naye kwa muda.

Katika mahojiano, alibainisha hawezi kaa peke yake ila akikataa katakata kumzungumzia mpenzi huyo wake na kusema hatoweka jina lake wazi..

“Safari hii NAMFICHA kama bangi... Ni 2023....Labda ata ni Bodyguard wangu na Hamumjui..  " Kyallo alisema kwa utani.

Mnamo mwezi Machi, mtangazaji huyo wa habari wa zamani alidokeza kwamba ni wakati sasa anahitaji kupata mtoto wa pili.

Katika mahojiano na wanablogu, Betty Kyallo alisema kwamba mtoto wake wa kwanza ambaye alizaa na mwanahabari mwenzake Dennis Okari kabla ya kutengana amekuwa akimpa shinikizo la kutaka ndugu.

Mwanahabari huyo alisema atang’ang’ana safari hii na kupunguza shinikizo hilo kwa kumzalia kifungua mimba wake ndugu.

“Kusema kweli ndio, nafikiri ni muda wa kufikiria kuongeza familia, mtoto. Ivana amekuwa akinipa shinikizo la kutaka dada, kaka. Nafikiri anahitaji mtu wa kumpa ushirikiano, nitamtafutia, nitang’ang’ana, Kyallo alisema.