Afungwa miezi 15 jela kwa kusumbua majirani kwa sauti ya juu ya muziki wa woofer

Isitoshe, lazima alipe faini ya Shilingi 351k na Shilingi milioni 2.9 za Kenya kama fidia kwa majirani zake na wale waliokerwa na kelele zake nyingi za kufanya mifupa kutetema katika kipindi cha miaka 5.

Muhtasari

• Ripoti zinasema majirani watatu waliokuwa wakiishi katika nyumba iliyounganishwa na ile ya mshtakiwa waliwasilisha malalamiko dhidi yake

• Walidai kuwa muziki huo wa kishindo ulikuwa ukiwadhuru kiakili na kimwili na hali zao za kiafya zilizidi kuwa mbaya.

Mahakama moja nchini Uhispania jimbo la Barcelona imemhukumu mwanamume kifungo cha miezi 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumpa jirani yake usumbufu kwa kucheza muziki kwa sauti ya juu kwa kipindi cha miaka 5.

Kwa mujibu wa jarida moda la Uhispania, jirani alielekea mahakamani kulalamika kwamba jirani huyo wake alikuwa anacheza muziki kwenye woofer yake kwa sauti za juu usiku na mchana bila.

Jirani huyo alisema kwenye hati ya malalamishi kwamba muziki huo ulikuwa wa juu kiasi kwamba alikuwa anahisi kama mifupa yake inatetema.

Ilithibitishwa kwamba mtu huyo aliwatesa majirani zake kimakusudi kwa kile ambacho ripoti fulani zilitaja kuwa ugaidi wa muziki kwa miaka mitano bila kukoma. Alishtakiwa kwa kucheza muziki usiku na mchana kati ya 2012 na 2017, na hata maombi ya majirani na maonyo ya polisi hayangeweza kumzuia.

Ripoti zinasema majirani watatu waliokuwa wakiishi katika nyumba iliyounganishwa na ile ya mshtakiwa waliwasilisha malalamiko dhidi yake mwaka 2015 baada ya kuvumilia kwa takriban miaka mitatu ya muziki wa sauti ya juu.

Walidai kuwa muziki huo wa kishindo ulikuwa ukiwadhuru kiakili na kimwili na hali zao za kiafya zilizidi kuwa mbaya.

Inaripotiwa kwamba vipimo vya sauti katika muda wote wa miaka mitano ya ugaidi wa sauti vilifichua kwamba muziki wa kielektroniki ulikuwa wa juu zaidi kuliko kiwango cha kisheria cha desibeli 35, ukizidi desibeli 57 mchana na jioni na desibeli 56 usiku.

Muziki huo uliripotiwa kuwa mkubwa sana hivi kwamba mali za wakazi wa karibu zilikuwa zikitetemeka mara kwa mara.

Baada ya kusikiliza ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani wa mshtakiwa na afisa wa polisi, mahakama ilimpiga kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitatu jela. Isitoshe, lazima alipe faini ya $2,417 [Shilingi 351k] na $20,000 [Shilingi milioni 2.9 za Kenya] kama fidia kwa majirani zake na wale waliokerwa na kelele zake nyingi.

"Kuendelea kwa mtazamo wake kunaonyesha kwamba mshtakiwa alifahamu kwamba mwenendo wake unaweza kuathiri utulivu wa kiakili wa jirani yeyote kwa sababu hata akiwa na ujuzi mdogo wa kijamii mtu hawezi ila kufahamu," hakimu alinukuliwa kusema.