Mrembo awatamanisha wengi kwa kuonyesha burunguti la pesa kwenye gunia (video)

Baadhi walisema kwamba ni hela ambazo amekuwa aki'save mwaka mzima kwa ajili ya kupiga sherehe msimu wa Krismasi miezi miwili ijayo.

Muhtasari

• “Wewe unatoa wapi pes azote hizo msichana mdogo, kwani huishi katika nchi moja kama sisi?” mwingine aliyesongwa na uchumi alimuuliza.

 

Mrembo na pesa nyingi.
Mrembo na pesa nyingi.
Image: TIKTOK

Mwanamke mmoja amewashangaza wengi kwa kupakia video ikionyesha pesa ambazo amekuwa aki’save kwenye gunia kwa ajili ya sherehe za Krismasi mwishoni mwa mwaka.

Katika video iliyoonekana kwenye TikTok, mwanamke huyo, @hoppy.fundz, alionyesha kwanza gunia kubwa lililo wazi lililojazwa mabunda kadhaa ya noti.

Alichukua mabunda kadhaa ya vifurushi na kupiga picha navyo. Kisha, alionekana akicheza na burungutu la pesa zilizotawanyika kitandani mwake.

Mwanamke mmoja alijiunga naye kwenye eneo la tukio walipokuwa na siku ya shambani wakiwa na pesa nyingi sana. Onyesho la mwanamke linakuja kabla ya siku yake ya kuzaliwa.

Baadhi ya watu walioona video hiyo walijawa na matamanio wengine wakimuomba kuwapa mgao kidogo.

Mrembo huyo alizua dhana mbali mbali kuhusu mtu kuwa na burunguti la ppesa taslimu nyumbani tena kwenye gunia enzi hizi ambapo wengi wanaweka pesa zao kwenye mifumo ya simu au benki.

Aidha wengine walisema kwamba hawawezi kuwa na Amani ya nafsi kuishi kwenye nyumba na pesa hizo taslimu kwani kila mara watakuwa na wasiwasi wa kufumaniwa na wezi na kuibiwa.

“Wewe huogopi kuishi na pesa za kiasi hicho taslimu kwenye nyumba, mimi siwezi pata hata lepe la usingizi kila mara nasikia hata panya akipita nasema wezi wamenifikia,” mmoja alishangazwa.

“Wewe unatoa wapi pes azote hizo msichana mdogo, kwani huishi katika nchi moja kama sisi?” mwingine aliyesongwa na uchumi alimuuliza.

“Enyewe dunia ya sasa ni bora kutafuta pesa kuliko elimu maana tulio na elimu tunaishi nayo kwa vichwa tu lakini maisha yanatutandika kwa umaskini,” mwingine alisema.