Kumalizia wikendi kwa nyumba ya jamaa au mrembo hujafunga ndoa naye ni dhambi - Pasta

“Unapaswa kuwaonya washiriki wa kanisa lako kwa mavazi yasiyofaa kwanza kabla ya kuja kwenye twitter kutoa ushauri. Upendo unaanzia nyumbani!” Big Smog alimtaka.

Muhtasari

• “Ni sehemu ya uchumba. Acha kujaribu kuwa mtakatifu sana. Utakatifu huu wa kujifanya unaua Ukristo,” Jet Daniel alimwambia.

Pasta aonya kulala kwa mtu hujaona naye
Pasta aonya kulala kwa mtu hujaona naye
Image: X

Mchungaji mmoja katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter, Bolaji Idowu amezua hisia mtandaoni kufuatia ujumbe wake wa hivi majuzi kwa wasenge ambao hawajafunga ndoa lakini wanaishi pamoja kama wanandoa.

Mchungaji huyo ambaye ibada zake nyingi huziandaa katika mitandao ya kijamii alilaani kitendo cha vijana wengi haswa wa vyuo vikuu ambao aghalabu siku za mwisho wa juma wanafunga safari kutoka mabweni yao kwenda kumalizia wikendi katika nyumba za wapenzi wao.

Mtu wa Mungu ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa Harvesters International Christian Centre huko mjini Lagos alisema kuwa wikendi ukiwa nyumbani kwa mwanamume au mwanamke ambaye hujafunga naye ndoa si jambo la kibiblia maana yake ni kutokuwa mtakatifu katika utakatifu unaotangazwa na injili ya Yesu kwa mitume wake.

Alifahamisha hili Oktoba 26, 2023 kwa wote na wengine kupitia ukurasa wake ulioidhinishwa kwenye jukwaa la X ambalo hapo awali liliitwa Twitter.

Mchungaji Bolaji Idowu aliandika; “Kutumia wikendi katika nyumba ya mwanamume/mwanamke ambaye hujafunga naye ndoa si jambo la kibiblia. Acha mara moja."

Kwa wazi, inajulikana kuwa siku hizi, waseja wengi tayari wanaishi pamoja kama wenzi wa ndoa bila utambulishaji wowote kwa familia zao bila kuzungumza juu ya harusi.

Mchungaji katika wadhifa wake hata hivyo anaamuru wale wanaohusika katika aina hiyo ya uchumba wakome sasa kwani aliiita dhambi, aina ya uzinzi.

Hata hivyo, licha ya wengi kuonekana kumuunga mkono, vijana wengi walimkomalia kwa kuwataka waache kile ambacho wana mazoea ya kukifanya.

“Ni sehemu ya uchumba. Acha kujaribu kuwa mtakatifu sana. Utakatifu huu wa kujifanya unaua Ukristo,” Jet Daniel alimwambia.

“Unapaswa kuwaonya washiriki wa kanisa lako kwa mavazi yasiyofaa kwanza kabla ya kuja kwenye twitter kutoa ushauri. Upendo unaanzia nyumbani!” Big Smog alimtaka.

“Mchungaji B, vipi ikiwa nitatumia Ijumaa usiku na kurudi nyumbani kwangu Jumamosi asubuhi lakini nikirudi Jumamosi jioni na sisi sote twende kanisani Jumapili asubuhi?” mwingine alimuuliza.

“Sijui nani anahitaji kusikia haya, usiwahi kufanya makosa kuoa mtu ambaye hujakaa naye wiki moja moja kwa moja,” mwingine alisema kwa utani.