Hisia mseto huku Andrew Kibe akiwatambulisha watoto wake baada ya kurejea Kenya

Kibe alionyesha picha yake na watoto wawili wazuri aliowataja kuwa matunda yake.

Muhtasari

•Kibe pamoja na watoto hao wawili, mvulana na msichana wote walionekana wakitabasamu ndani ya gari la kibinafsi.

•Wakenya walipokea posti hiyo kwa hisia tofauti huku kundi likionekana kushangazwa baada ya kujua kwamba ana familia.

Image: TWITTER// ANDREW KIBE

Siku ya Jumanne, mtangazaji maarufu wa Kenya Andrew Kibe alichapisha  picha yake nzuri akifurahia muda mzuri na watoto wake wawili.

Katika picha hiyo, Kibe ambaye amekuwa akiishi Marekani katika miezi ya hivi majuzi pamoja na watoto hao wawili wadogo, mvulana na msichana wote walionekana wakitabasamu ndani ya gari la kibinafsi.

Kwenye sehemu ya maelezo ya picha hiyo, mtangazaji huyo wa zamani wa redio aliwatambulisha watoto hao wazuri kama matunda yake.

"Na matunda ya mwili wangu," Kibe aliandika kwenye Twitter.

Wakenya walipokea posti hiyo kwa hisia tofauti huku kundi likionekana kushangazwa baada ya kujua kwamba mtangazaji huyo ambaye amesikika kuwa na sauti kubwa kuhusu ndoa na mahusiano ana familia huku wengine wakionekana kumpongeza.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya;-

@kijanaYaa: Kwa hiyo uko na watoto bado unakatisha tamaa watu kuoa!

@ArchLibwege: Mama yao yuko wapi?

@muli_brian: Umefanya DNA?

@mwangi_kevinne: Ninaweza kufikiria jinsi walivyofurahi kutumia wakati na baba yao.

@Burgermoyoo: Kibe kweli ni baba na kulea binti? Naah jamaa.

Tangu kuacha kazi yake ya utangazaji wa redio na kuhamia nje ya nchi, Andrew Kibe amekuwa akiendesha Podcast ambapo amekuwa akizungumzia mengi kuhusu uwezeshaji wa wanaume na kufundisha wanaume jinsi ya kukabiliana na wanawake na mahusiano.

Mzungumzaji huyo maarufu mwenye utata mwingi pia amekuwa akiwaonya wanaume kuhusu shida mbali mbali zinazopatikana katika ndoa na kuwataka kila wakati kufanya DNA kwa watoto wanaozaliwa.

Andrew Kibe alirejea nchini Kenya siku ya Ijumaa kabla ya hafla ya uzinduzi wa programu yake iliyofanyika wikendi. Alipokelewa na baadhi ya mashabiki wake katika Uwanja wa Ndege wa JKIA na alionekana akitabasamu huku akitafuna chingamu.

Mtangazaji huyo ambaye alikuwa amevalia miwani mieusi na kujifunika sehemu ya uso wake na kuacha uso peke yake alikuwa na walinzi waliomsindikiza hadi kwenye gari lililokuwa likimsubiri kisha wakaondoka.