Wapenzi Grand P na Eudoxie Yao hatimaye wafichua jinsi wanavyoshiriki tendo la ndoa

Mwanasosholaiti Eudoxie Yao alibainisha wazi kwamba wanaridhishwa na matukio yao ya mapenzi.

Muhtasari

•Walisema kwamba mchezo wao wa kitandani ni wa kuridhisha ila walisusia kushiriki maelezo zaidi kuhusu jinsi wanavyofanya.

•Grand P alisema anafurahishwa na mwanasosholaiti huyo na akadokeza kuwa atamuoa rasmi atakapokuwa tayari kwa hatua hiyo.

Image: HISANI

Wanandoa maarufu wa Afrika Magharibi, Grand P na mkewe Eudoxie Yao, katika mahojiano ya hivi majuzi walilazimika kueleza jinsi maisha yao ya mapenzi yalivyo ikizingatiwa kwamba kuna tofauti kubwa sana katika saizi ya miili yao. 

Wanandoa hao ambao walizungumza na Joy Prime TV wakati wa ziara yao nchini Ghana walisema kwamba mchezo wao wa kitandani ni wa kuridhisha lakini walisusia kushiriki maelezo zaidi kuhusu jinsi wanavyofanya.

 "Maisha yetu ya mapenzi ni ya kuridhisha, lakini tunapendelea kuweka maelezo ya faragha," Eudoxie Yao alisema.

Grand P ambaye anatambuliwa zaidi kwa mwili wake mdogo wa kipekee na sauti ya mtoto kwa upande wake hata hivyo kutoa maoni kuhusu maisha yao ya mapenzi. Hata hivyo alibainisha kuwa anafurahishwa na mwanasosholaiti huyo wa Ivory Coast na akadokeza kuwa atamuoa rasmi atakapokuwa tayari kwa hatua hiyo.

Katika mahojiano hayo, Eudoxie Yao alimshtumu mpenziwe kwa kupenda wanawake sana na kumsaliti kimapenzi mara kadhaa.

Mwanasosholaiti huyo alidai kuwa Grand P ana tabia ya kuwamezea mate wanawake wengine, jambo ambalo limemfanya amuache mara kadhaa wakati wa uhusiano wao.

"Tumechumbiana tangu 2019. Tunaachana, Tunarudiana. Tunaachana tena na kurudiana.. Anapenda wanawake sana,” Grand P alisema katika mahojiano na Joy News.

Grand P hata hivyo alikuwa mwepesi sana kukanusha madai ya kuwapenda wanawake sana.

"Hapana! Hapana! Ni Mungu pekee ndiye anayejua,” Grand P alisema.

Huku akizungumzia uhusiano wao, Bi Yao aliweka wazi kuwa licha ya wao kutofunga ndoa rasmi, upendo  ni wa kweli kabisa.

Wakati wa mahojiano, Grand P ambaye ni Muislamu hata hivyo alifichua kuwa nia yake ni kuoa takriban wanawake wanne.

“Nataka kuoa wanawake wanne. Si mimi niliyesema hivyo, ni baba yangu (Mungu) anayesema hivyo,” alisema.

Eudoxie Yao hata hivyo alikuwa mwepesi wa kutokubaliana na wazo hilo akisema, "Ikiwa atathubutu, tunaachana."