"Sio ukubwa unaomfanya mwanaume mkuu!" Grand P asema huku akizama kabisa katika mapenzi

Grand P aliandamana na Zhang hadi kwenye duka la urembo ambako walitengezwa nyuso.

Muhtasari

•Katika taarifa yake, Grand P aliwakumbusha watu kuwa ubora wa mwanaume haupimwi kwa ukubwa wake.

•Wapenzi hao walianza kuchumbiana miezi kadhaa baada ya mahusiano ya Grand P na Eudoxie Yao kufika kikomo.

Grand P, Eudoxie Yao, Yubai Zhang
Image: HISANI

Mahaba ya mwimbaji mashuhuri wa Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P na mpenzi  wake mpya Yubai Zhang yameendelea kupamba moto.

Grand P alimtambulisha mrembo huyo mwenye asili ya Asia kama mpenziwe mpya mapema mwaka huu, takriban mwaka mmoja baada ya kutengana na mwanasosholaiti wa Ivory Coast mwenye umbo wa kustaajabisha, Bi Eudoxie Yao.

Wikendi, msanii huyo mwenye maumbile ya kipekee aliandamana na Bi Zhang hadi kwenye duka la urembo ambako walitengezwa nyuso. Wawili hao walichapisha picha kadhaa ambazo zilipigwa wakati wa kipindi cha kurembeshwa.

"Oooh, mzuri aje mpenzi wangu Grand P. Mume wangu," Bi Zhang alisema kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Katika taarifa yake, Grand P aliwakumbusha watu kuwa ubora wa mwanaume haupimwi kwa ukubwa wake.

"Sio ukubwa unaomfanya mwanaume kuwa bora 💪💪 Matibabu ya uso kwa kukutana na mpenzi wangu Yubaï Zhang," alisema.

Mwimbaji huyo aliambatanisha taarifa hiyo na video iliyomuonyesha akitengenezwa uso na mtaalamu wa urembo.

akitengenezwa uso.
Grand P akitengenezwa uso.
Image: HISANI

Grand P alimtambulisha mpenzi huyo wake mpya mapema mwezi jana na wawili hao wamekuwa wakijivanjari pamoja na kuonyesha muungano wao mzuri. Mapema mwezi huu, mwanamuziki huyo mwenye ufuasi mkubwa alijigamba  kuhusu mapenzi matamu ambayo amekuwa akipewa na kipusa huyo.

"I am a spoiled baby by Yubai Zhang❤," alisema kwenye picha yake na Zhang aliypchapisha kwenye Instagram.

Kumaanisha, "Mimi ni mtoto aliyeharibiwa."

Katika chapisho lingine, alithibitisha mapenzi yake na mrembo huyo  na kuweka wazi hakuna nafasi ya watu wenye wivu maishani mwao.

"Yubai Zhang wangu, hakuna nafasi kwa watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang alizochapisha Facebook.

Mwimbaji huyo maarufu na mpenziwe mpya wamekuwa wakisafiri katika nchi tofauti pamoja na kujivinjari pamoja katika sehemu mbalimbali. Wawili hao hawajaona haya kukiri mapenzi yao mazito licha ya tofauti zao.

Wapenzi hao walianza kuchumbiana miezi kadhaa baada ya mahusiano ya Grand P na mwanasoshalaiti wa Ivory Coast mwenye umbo la kustaajabisha kweli, Eudoxie Yao  kufika kikomo mapema mwaka jana kwa njia isiyoeleweka baada ya wawili hao kuchumbiana kwa takriban miaka mitatu.