Mke achangiwa zaidi ya 2m mtandaoni kwa kukiri kurauka 4am kila siku kumpikia mumewe

Debbie alitema upande wake wa hadithi katika ndoa, bila kujua kwamba hadithi hiyo ndiyo ingekuwa kichocheo cha mabadiliko makubwa ya maisha yake.

Muhtasari

• Debbie alisema kwamba yeye zamani hakuwa anafanya hivyo lakini baada ya kuambiwa kwamba mumewe alikuwa anategemea chakula cha mfanyikazi mweza kazini, alijichuna sikio na kuweka alarm kumuamsha 4:50am kila siku.

Debbie
Debbie
Image: x

Mwanamke mmoja amelala na kuamka na bahati ya mtende baada ya kushiriki simulizi yake jinsi alianza kurauka kila siku saa kumi alfajiri kwa ajili ya kumtayarishia mumewe chakula kabla ya kwenda kazini.

Mwanamke huyo kwa jina Debbie katika mtandao wa X alikuwa anajibu swali la mtumizi mmoja wa mtandao huo ikiwa kaitka dunia ya sasa kuna mwanamke anayeweza kurauka kila siku alfajiri kwa ajili ya kumpikia mumewe kabla ya kwenda kazini.

Debbie alitema upande wake wa hadithi katika ndoa, bila kujua kwamba hadithi hiyo ndiyo ingekuwa kichocheo cha mabadiliko makubwa ya maisha yake.

Debbie alisema kwamba yeye zamani hakuwa anafanya hivyo lakini baada ya kuambiwa kwamba mumewe alikuwa anategemea chakula cha mfanyikazi mweza kazini, alijichuna sikio na tangia hapo aliweka alarm kumuamsha kila siku 4:50am kumpikia mumewe kabla ya kwenda kazini.

“Nilikuwa mvivu sana kuamka na kuandaa chakula chake cha mchana. Lakini siku ambayo aliniambia mfanyikazi mwenza alileta vijiko viwili ili akule naye, ndiyo siku ambayo niliweka alarm yangu ya 4:50 asubuhi,” Debbie alisema.

Kutokana na kukiri huko, wanamitandao wengine walimtupia maneno ya kumsimanga kwa kujifanya kuwa mtumwa katika ndoa lakini kuna baadhi waliomsifia kama shujaa wa ndoa na kumuomba aweke namba yake kwa ajili ya kumchangia hela za kumliwaza kwa kuonesha mfano wa kielelezo bora katika ndoa.

Ndani ya siku chache, Debbie ameripotiwa kupokea Zaidi ya Naira milioni mbili za Kinaijeria, sawa na takribani laki nne za Kenya.

Mrembo huyo alirudi kwenye mtandao wa X na kuchapisha picha na miamala ambayo amepokea na kuwashukuru wote waliojitolea kumhongera kwa njia ya pesa baada ya kushiriki hadithi yake ya ujasiri.

“Kwa kila aliyehusika na hili, sina maneno, lakini nimelia moyo wangu kwa maombi kwa kila mtu aliyechangia, kupost na kunitakia heri. Kichwa kinaniuma na nataka kulala tu. Asanteni sana wote,” alisema.