Samsom mwingine? Jamaa ashangaza watu kwa kupambana na simba sebuleni (video)

Awali, jamaa huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwahi kuonekana akimenyana kwa ujasiri na chatu mwenye urefu wa futi 18 na kumshinda.

Muhtasari

• Kipande hicho kikiendelea, simba alionekana kutaka kutoka kwenye blanketi na kumkabili mwanamume huyo.

Jamaa akikabiliana na simba.
Jamaa akikabiliana na simba.
Image: Screengrab

Mwanamume mmoja raia wa Afrika Kusini amewashangaza wartu baada ya video yake kuibuka mitandaoni ikimuonyesha jinsi alivyokuwa akipambana na simba dume katika sebule ya nyumba yake.

Video iliyoshirikiwa kwenye Facebook na @Bokkeboys ilionyesha mwanamume huyo akipigana mieleka na simba.

Mwanaume huyo ambaye alionekana kama anafanya mchezo na mnyama huyo hatari mfalme wa porini, alionekana akimrukia mgongoni huku akijaribu kumfunika kichwa chake kwa kutumia blanketi kwenye kochi.

Kipande hicho kikiendelea, simba alionekana kutaka kutoka kwenye blanketi na kumkabili mwanamume huyo.

Video inaendelea kwa kumuonyesha mwanaume huyo na simba wakiwa wamelala chini. Vitendo vya mwanamume huyo shupavu vilifanya ndimi zitetemeke, huku mtu mmoja akisema kwenye maoni:

“Hii inaweza kutokea Afrika Kusini pekee kwa kweli.”

Ingawa kutazama mwanamume huyo akipigana mweleka na simba kulikuwa kufurahisha kwa watu wengine, baadhi walihisi kwamba ilikuwa kupita kiasi.

Inaarifiwa kwamba hii si mara ya kwamba kwa mwanamume huyo anayetajwa kuwa mkulima na mfugaji wa wanyama hatari kuonekana akifanya mchezo na wanyamapori.

Awali, jamaa huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwahi kuonekana akimenyana kwa ujasiri na chatu mwenye urefu wa futi 18 na kumshinda.

Taarifa kutoka Kanda ya Kati lilikotokea tukio hilo zinaeleza kuwa nyoka huyo mkubwa alikuwa amemzunguka mbwa akivunja mifupa yake wakati mkulima huyo alipofika eneo la tukio.

Kwa panga lake, alimshambulia nyoka huyo hadi hatimaye akamshinda na kumwachilia mnyama wake mwaminifu wa shambani.