Pasta awapa changamoto wakristo kuweka mishahara yao ya Januari kwa akaunti yake (video)

Kulingana naye, pesa hizo ni kwa ajili yake na si za kanisa na kuongeza kuwa wanapaswa kuhakikisha wanazituma kwani wataona maajabu hivi karibuni.

Muhtasari

• Kulingana naye, pesa hizo ni kwa ajili yake na si za kanisa na kuongeza kuwa wanapaswa kuhakikisha wanazituma kwani wataona maajabu hivi karibuni.

PASTA JOHN ANOSIKE
PASTA JOHN ANOSIKE
Image: FACEBOOK

Zikiwa zimesalia takribani wiki mbili kuelekea mwisho wa mwezi wa Januari – unaotajwa kuwa mrefu na wenye mateso Zaidi kwa watu wengi, wengi wanatarajia kupata mishahara, tayari kuna mchungaji ameanza kupigia hesabu mishahara ya waumini wake.

Video ambayo imewaghadhabisha wengi mitandaoni inamuonyesha mchungaji mmoja kutoka Nigeria aliwapa changaoto waumini wa kanisa lake kuweka mishahara yao yote ya mwezi Januari kwenye akaunti yake.

Katika video hiyo inayoenezwa mtandaoni, Mchungaji huyo aliyetambulika kwa jina John Anoskie anawaambia waumini wa kanisa lake walipe matunda yao ya kwanza ya mwaka inayojulikana kama mishahara yao kwenye akaunti yake.

Kulingana naye, pesa hizo ni kwa ajili yake na si za kanisa na kuongeza kuwa wanapaswa kuhakikisha wanazituma kwani wataona maajabu hivi karibuni.

Kwa maneno yake; “Nataka nikupe changamoto kwa Roho wa Mungu, siogopi mtu wala lawama, ukiniita Baba yako wa kiroho, mshahara wa mwezi huu, limbuko lako la mwaka, ni kwangu, si kwa kanisa, ni kwa ajili hii. kubadilisha, neno, ni kwa ajili ya ustawi wangu."

Akiongea zaidi, pasta huyo alikerwa kuwa iwapo waumini wa kanisa hilo watamtii kwa kumheshimu kwa mishahara yao ya Januari, wataona mabadiliko makubwa katika maisha yao ifikapo katikati ya mwaka huu.

Anaendelea kuwa ikiwa hawawezi kushuhudia au kuona mabadiliko yoyote makubwa katika maisha yao, wanapaswa kurudi na atawarudishia pesa zao.

Katika kile kinachoonekana kuwa tishio, pasta alihitimisha kwamba ikiwa washiriki wa kanisa hilo walimwona kuwa baba yao, mchungaji, mshauri, na ikiwa walikuwa wana na binti za kanisa wanapaswa kuhakikisha wanatuma pesa kwenye akaunti yake inayoonyeshwa kwao.

Hii inaambatana na video ya hivi majuzi ya pasta Victor Kanyari ambaye pia alikuwa anawazomea waumini ambao walikuwa na mazoea ya kwenda kumuona mikono mitupu.

Katika video hiyo ya Kanyari, aliwasuta waumini wanaomchukulia kama baba yao wa kiroho lakini nyakati za kwenda kumuona wanajikokota mikono mitupu au na shilingi 200 hadi 500, kiasi ambacho kwake hakifai hata kidogo.

Alisema kwamba ataanza kuwafukuza kanisani waumini wanaokwenda kumuona bila kubeba bidhaa za kula kama vile sukari, majani na vingine.